Tuesday May 3, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Waathirika wa mabomu Mbagala kuandamana Ikulu

9th May 2012
Print
Comments
Rais Jakaya Kikwete

Wakazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam walioathirika na mlipuko wa mabomu, wameandaa maandamano ya amani kuelekea Ikulu kuonana na Rais Jakaya Kikwete kwa lengo la kushinikiza kulipwa malipo yao ya uharibifu wa nyumba zao.

Mwenyekiti wa kamati ya waathirika hao, Steven Gimonge, alisema wamejipanga kuandamana ili Rais Kikwete awahoji watendaji wake waliopewa jukumu la kuwalipa kutofanya hivyo.

“Baada ya kufanya juhudi zetu za kukutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kushindikana tangu Februari, 2010, sasa tumeamua kuandaa maandamano ya amani hadi Ikulu kuonana na Rais,” alisema.

Akiwa ameongozana na katibu wa katibu hiyo, Laurent Nyiga na Eligius Mbonde (mjumbe), alisema wanawakilisha zaidi ya wakazi 2,000 ambao miongoni mwao walilipwa fedha zisizoendana na thamani ya majengo yao na wengine hawakulipwa kabisa.

Alisema serikali imewatelekeza na kuwaacha wakiwa ndani ya nchi yao baada ya kusambaratishwa na mabomu hayo Aprili 29, 2009, hali ambayo iliyowafanya kumtafuta Waziri Mkuu na kushindikana.

Walisema wamepanga kuandamana hadi Ikulu baada ya kuona Rais Kikwete aliyewatembelea baada ya tukio hilo, kuwaahidi kuwalipa hadi kijiko kilichopotea, lakini haihawa hivyo mpaka sasa.

“Wakati ule tulisikia tumeletewa simenti, mabati, magodoro na mablanketi, lakini hajaona chochote kile kwa waathirika, na kuhusu fidia ya nyumba zetu, jambo hilo ndilo linazungushwa mpaka wakati huu,” alisema.

Hata hivyo, Gimonge alisema walifanya juhudi  za kufanikisha kupata fidia, lakini walishindwa kuambiwa lolote na wahusika akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati ule, William Lukuvi.

“Ili kuonana na Pinda, tulipata msaada toka kwa mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, kwa kutuandika barua yenye kumb. MNF/AD/3 ya Januari 29, 2010…lakini juhudi hizo za kuonana na Waziri Mkuu zimegonga mwamba hadi leo,” alisema Gimonge.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles