Friday May 24, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Dk. Shain asisitiza umuhimu kwa wananchi kujulishwa ufanisi wa TVZ

20th May 2012
Print
Comments
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein alisema wananchi wana haki ya kupewa taarifa juu ya sababu za matangazo ya Kituo cha Televisheni Zanzibar (ZBC) kukosa uhakika wa kupatikana kisiwani Pemba.

Dk Shein akizungumza na watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo mjini hapa jana alisema ni jukumu la viongozi ZBC kueleza matatizo ya chombo hicho kila yanapojitokeza.

Dk Shein alitoa tamko hilo katika mkutano wake na watendaji wakuu wa wizara hiyo chini ya utaratibu aliojiwekea wa kuangalia utekelezaji wa mpango kazi kwa kila wizara.

Alisema kwamba hatua ya kuwafahamisha wananchi ni jambo la msingi na kuwataka kuhakikisha wanafanya juhudi za haraka kurekebisha hali hiyo.

Dk. Shein akizungumzia ukarabati wa jengo la zamani la studio ya kurekodi muziki kilichopo Rahaleo, alisema hatua hiyo ni muhimu kwa sababu itasadia kuendeleza vipaji vya wasanii wa taaluma ya muziki na sanaa na kuongeza ajira kwa vijana visiwani.

Aidha, Dk. Shein alisisitiza haja kwa watendaji na viongozi wa serikali kuandaa ripoti juu ya safari zao za kikazi wanazokwenda ndani na nje ya Zanzibar ili ripoti hizo ziweze kusaidia katika uharakishaji wa maendeleo ya nchi.

Pamoja na mambo mengine Dk. Shein alieleza azma ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya kuweka mtambo mpya wa kuchapisha vitabu vya bajeti, nyaraka za serikali pamoja na mtambo mkubwa kwa ajili ya kuchapishia magazeti.

Vile vile alieleza haja ya kutengeneza Filamu inayozungumzia maendeleo ya Zanzibar ili wananchi waweze kujua hatua za maendeleo zinazochukuliwa SMZ katika utekelezaji wa mpango wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa wananchi wake.

Mapema Waziri wa Wizara hiyo Said Ali Mbarouk, alisema kuwa Baraza la Kiswahili limefanya tafiti kwa wasanii waliofariki miongoni mwa hao ni marehemu Bakari Abeid, Iddi Abdalla Farhani na Issa Haji Pandu (Issa Matona) kwa malengo ya kuweka kumbukumbu zao.

Mbarouk, alisema kwamba pia Wizara hiyo imeanza utaratibu wa kupasha habari kwa njia ya ishara ili kuwapatia fursa watu wenye mahitaji maalumu.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment