Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Upinzani ukituzidi tutawatumia Mwinyi, Mkapa-Kinana

22nd September 2010
Print
Comments
Mwenyekiti wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi

Mwenyekiti wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa watashiriki kampeni za Rais Jakaya Kikwete iwapo kitazidiwa na upinzani.

Taarifa ya Kinana ilitolewa jana kwa niaba yake na mjumbe wa kamati ya kampeni za CCM, Dk. Raphael Chegeni alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Kinana alisema hali ya kampeni ilivyo sasa inaashiria kuwa mambo yanakwenda vizuri.

"Sio kwamba mgombea wetu ametengwa na marais wastaafu, tunaona chama hakijazidiwa na wapinzani hivyo hakuna sababu ya kuwasumbua mzee Mwinyi na Mkapa," alisema.

Pia alisema CCM inamtambua mshindi wa kura za maoni kuwania ubunge wa jimbo la Nzega mkoani Tabora, Hussein Bashe.

Bashe alishinda kura za maoni lakini Kamati Kuu (CC) ya CCM ilimuengua kwa kile kilichodaiwa kwamba si raia wa Tanzania.

Alisema CCM ipo tayari kumtumia Bashe katika shughuli mbalimbali za chama, ikiwemo kusaidia kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles