Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Daruso wataka sababu za wenzao kufukuzwa

11th February 2011
Print
Comments

 

Uongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso), umepeleka maombi kwenye uongozi wa chuo hicho, kuomba kurudishwa mapema wanafunzi 1200 wanaochukua Shahada za kwanza katika Koleji ya Uandisi na Teknolojia ambao waliosimamishwa juzi.

Wanafunzi hao walisimamishwa baada ya kufanya vurugu na kuwatisha wahadhiri ili kuushinikiza uongozi huo umrudishe chuoni mwanafunzi mwenzao Jamson Babala aliyefukuzwa baada ya kubainika akiibia mtihani.

Waziri Mkuu wa Chuo hicho, Paul Makuli, aliliambia gazeti hili jana kuwa, wameomba uongozi huo kuwarudisha wanafunzi hao mapema na kujua masharti waliyotoa kwao.

"Kwa kawaida mwanafunzi anaposimamishwa lazima apewe masharti lakini hawa hawajapewa, tunataka kujua masharti hayo na ni lini watarudishwa chuoni," alisema.

Pia alisema wanatarajia kuuomba uongozi huo, usitoe masharti magumu yatakayowafanya wanafunzi washindwe kuyatimiza.

Wakati huo huo, wanafunzi waliosimamishwa hadi kufikia jana walikuwa wameondoka chuoni hapo kwa nyakati tofauti.

Hata hivyo, NIPASHE iliwashuhudia wanafunzi wengine waliokuwa wamefanya mgomo wakishinikiza waongezewe fedha za kujikimu kutoka shilingi Sh. 5,000 hadi 10,000 wakijisomea kujiandaa na mitihani ya majaribio inayoendelea chuoni hapo.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles