Thursday May 23, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Balozi: Jaji Ramadhani alifuata maadili

24th February 2012
Print
Comments
Mkuu mstaafu, Augustino Ramadhani (kushoto), kwenye Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni mke wa Jaji Ramadhani, Luteni Kanali, Saada Mbarouk. (PICHA: KHALFAN SAID)

Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt, amewaasa viongozi walioajiriwa kwenye ofisi za umma kutozitumia kwa ajili ya ufisadi, badala yake wazitumie kuwahudumia wananchi kwa haki wakiongozwa na maadili ya utumishi kama alivyofanya Jaji MKuu Mstaafu, Augustino Ramadhani, wakati wa utumishi wake.

Balozi Lenhardt aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kumtunuku J aji Ramadhani, Tuzo ya Haki ya Dk. Martin Luther King kwa mwaka 2012.

“Maisha ya Jaji Mkuu mstaafu Ramadhani katika utumishi wake wa serikali na mchango alioutoa wa kuwa sauti ongozi kwa hitaji la kuwahakikishia wanawake fursa ya kupata haki na umiliki wa mali unaakisi kwake moyo na urithi wa Martin Luther King na ndiyo kigezo kilichomfanya tumutunukie tuzo hii,” alisema.

Alisema pamoja na kuwa Jaji Ramadhani amestaafu, lakini bado ameendelea kukuza uwazi serikalini ili kulinda kanuni za haki na uwajibikaji wa umma ili kujenga demokrasia nchini na kuaminika kwa taasisi za umma mbele ya wananchi. Jaji Ramadhani alilaani kitendo kinachofanywa na polisi cha kuwaweka watu ndani kwa zaidi ya saa 24 bila ya kuwapeleka mahakamani.

Alisema kwamba kitendo hicho ni kinyume cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Kifungu Namba 32(1) ambacho kinaharamisha kitendo hicho na kutoa mamlaka kwa Mkuu wa Kituo (OCS) kumuachia mtu aliyekaa ndani kwa zaidi ya masaa 24.

Jaji Ramadhani aliwaasa wakuu wa vituo nchini kutumia kifungu hicho kuwaachia wananchi wote waliowekwa ndani kwa zaidi ya masaa 24 bila ya sababu za msingi, kwa kuwa kitendo hicho ni cha kuwanyima haki ya kisheria wananchi.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment