Sunday May 26, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Coastal wamnasa Chove

19th June 2012
Print
Comments
Kipa wa zamani wa Azam, Jackson Chove.

Klabu ya Coastal Union ya Tanga imetangaza kusajili wachezaji kadhaa akiwemo kipa wa zamani wa Azam, Jackson Chove.

Afisa Habari wa Coastal, Eddo Kumwembe, aliiambia NIPASHE kuwa Chove ni miongoni mwa makipa wawili wapya iliyowasajili kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kumwembe alimtaja kipa mwingine watakayemsajili ni Juma Mpongo aliyekuwa akiidakia Kiyovu Sports ya Rwanda.

Aliwataja wachezaji wengine waliowapata ni mshambuliaji Nsa Job kutoka Villa Squad, mlinzi wa kushoto wa JKT Oljoro, Othman Omary na Atupele Green aliyekuwa Yanga na timu ya taifa ya U20.

Wengine ni Soud Mohamed kutoka Toto, Seleman Kassim Salembe na Razaq Khalfan waliokuwa African Lyon.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment