Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Ujenzi wa mji mkongwe Dar kuanza Mei

11th February 2013
Print

Mradi wa ujenzi wa nyumba katika eneo la mji mkongwe lililoko Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni, mkoani Dar es Salaam utaanza mwishoni mwa Mei, mwaka huu.

 
Mratibu Uwekezaji wa Manispaa hiyo, Einhard Chidaga, aliiambia NIPASHE  kuwa mchakato wa kupata wawekezaji uko kwenye hatua za mwisho kwa kuwa tayari walioomba wameshaainishwa na Kamati ya Fedha ya Manispaa na kinachofuata ni kupata mapendekezo ya kiufundi na kifedha kutoka kwa wawekezaji hao.
 
“Tunataka kuzikamilisha taratibu zote za manunuzi kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ili tuanze ujenzi mapema kwani ndiyo mojawapo ya changamoto zinazotukabili kwa hivi sasa,” alisema.
 
Aidha, Chidaga alisema manispaa inataka kuanza ujenzi mapema ili waliokuwa wapangaji wao warejee kama walivyokubaliana katika mkataba baina yao. Eneo linalotarajiwa kujengwa mradi huo lina ukubwa wa ekari 31.2 na limepimwa katika viwanja vitatu ambavyo ni namba 1000, 1001 na 1002 kitalu ‘R’. Lilikuwa na nyumba 644 zilizokadiriwa kuwa na wakazi 2,000. 
 
Manispaa ya Kinondoni ilizivunja nyumba hizo zilizokuwa zimechakaa kwa ajili ya kuendesha mradi wa ujenzi wa majengo ya kibiashara na makazi yatakayokuwa na  huduma mbalimbali zikiwamo ofisi, huduma za kijamii, kumbi za mikutano, afya, maegesho, bustani na makazi ya juu, kati na chini.
 
SOURCE: NIPASHE

Articles

No articles