Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mfumuko wa bei wapungua

9th May 2013
Print
Nyanya zikiwa sokoni

Mfumuko wa bei za bidhaa nchini umepungua kutoka asilimia 9.8 mwezi Machi hadi 9.4 mwezi uliopita, isipokuwa kwa bidhaa ya nishati kutokana na uwezo wa Shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma kuendelea kupungua.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraimu Kwesigabo, wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa thamani ya shilingi ya Tanzania inatafsiriwa kuwa ni badiliko la uwezo wa shilingi katika kununua bidhaa na huduma zile za mlaji.

Kwesigabo alisema ikiwa wastani wa faharisi za bei za Taifa umeongezeka, uwezo wa shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma hupungua.

Aidha, alisema badiliko la fahirisi ya bei za bidhaa za vyakula majumbani na migahawani umepungua hadi asilimia 9.7 Aprili  ikilinganishwa na asilimia 10.7 ya Machi.

Aliongeza kuwa bei ya bidhaa zisizo za vyakula imeongezeka hadi asilimia 8.7 kwa Aprili kutoka asilimia 8.5 mwezi Machi, mwaka huu.

Alifafanua kuwa bidhaa zisizo za vyakula zimechangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa kipindi cha mwezi ni bidhaa za pombe kali kwa asilimia 0.5 na viatu kwa asilimia 0.3, mafuta ya taa kwa asilimia 1.6, mkaa kwa asilimia 3.6, petroli kwa asilimia 1.7 na nauli za daladala kwa asilimia 16.9.

Alisema mfumuko wa bei za vyakula wa bidhaa na huduma zote isipokuwa bidhaa za vyakula vya nishati haijumuishi vyakula vinavyoliwa nyumbani na migahawani, vinywaji baridi, petroli, dizeli, gesi ya kupikia, mafuta ya taa, mkaa na umeme.

Alifafanua kuwa vyakula na nishati vina sifa ya kuwa na bei  ambazo hubadilika mara kwa mara hivyo vikiondolewa kwenye faharisi ya bidhaa na huduma zote hubaki faharisi ambayo inamwelekeo imara.

Alisema mfumuko wa bei umekuwa na mwenendo wa kushuka kutoka asilimia 18.7 mwezi Aprili hadi kufikia asilimia 9.4 Aprili mwaka huu.


 

SOURCE: NIPASHE

Articles

No articles