Friday Apr 29, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Washambuliaji wa4 wamridhisha Kibadeni

13th July 2013
Print
Abdallah 'King' Kibadeni

Kocha wa klabu ya Simba, Abdallah 'King' Kibadeni, amesema safu yake ya ushambuliaji imekamilika na ameridhishwa na kiwango cha Koipou Felix, Kun James, Betram Mombeki na Ramadhan Singano 'Messi'.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kibadeni alisema wachezaji hao wameonyesha uwezo mkubwa na ushirikiano wa hali ya juu wawapo uwanjani.

"Bado naendelea kuangalia nani acheze na nani ... lakini nimeridhishwa na uwezo wao hasa hawa wachezaji watatu wageni," alisema Kibadeni.

Alisema kuwa hajajua wachezaji gani atakuwa akiwaanzisha katika safu hiyo kwa kuwa wote wanalingana kwa uwezo.

Aidha, alisema kuwa kwa kiasi kikubwa programu yake imefanikiwa hasa baada ya kujua mfumo atakaokuwa akitumia.

"Kikosi changu cha kwanza nitakijua baada ya wachezaji waliopo kwenye kambi ya timu ya taifa watakapoungana na sisi," alisema zaidi Kibadeni.

Aidha, alisema kuwa michezo ya kirafiki wanayocheza inamsaidia kujua zaidi uwezo wa wachezaji wake baada ya kuwaona kwenye mazoezi ya timu hiyo.

Alisema kuwa mchezo ujao wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya URA ya Uganda utakuwa kipimo kizuri kwa timu yake kuelekea kuanza kwa ligi kuu msimu ujao.

Simba inatarajia kucheza na URA Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo kikosi cha timu hiyo ya Uganda kinatarajiwa kuwasili nchini Jumatano.
 

SOURCE: NIPASHE

Articles

No articles