21 Jul 2005 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wawili wafa katika ajali
 
2005-07-21 14:49:44
Na Mwanaidi Swedi, Polisi Kati

Watu wawili wameaga dunia katika matukio mawili tofauti ya kugongwa na gari katika barabara za Mandela na Kawawa, Jijini.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Dar es Salaam, Alfred Tibaigana amesema tukio la kwanza limetokea katika barabara ya Mandela juzi saa 11:00 jioni, wakati gari lenye namba za usajili T 381 AGR lilipomgonga mtoto Omari Ramadhani wakati akijaribu kuvuka barabara maeneo ya gereji ya Mabibo External.

Kamanda Tibaigana amesema dereva wa gari hilo aliyekuwa akitokea Ubungo kwenda Buguruni baada ya kusababisha ajali hiyo, alikimbia na hakuweza kupatikana.

Hata hivyo Kamanda amesema vijana wake wanaendelea kumsaka.

Amesema tukio la pili limetokea huko maeneo ya Bonde la Mkwajuni Kinondoni, saa 2:00 usiku wakati gari lisilofahamika namba zake wala aina, lilipomgonga na kumuua mwenda kwa miguu anayekadiriwa kuwa na miaka 30 na 35.

Kwa maelezo ya Kamanda Tibaigana, marehemu alikuwa amevaa suruali ya kadeti na t-shirt ya kijani na jina lake halikuweza kupatikana mara moja.

Amesema miili ya marehemu hao imehifadhiwa chumba cha maiti cha hospitali ya Taifa Muhimbili.

Wakati huohuo, moto mkubwa umetokea jana saa 8:00 mchana huko Manzese katika nyumba ya Tatu Hussein, 47, na kuteketeza kila kitu.

Kamanda Tibaigana amesema chanzo cha moto huo ni kibatari kilichowashwa na mjukuu wa mama huyo mwenye umri wa miaka minne.

Hata hivyo pamoja na kikosi cha Zimamoto, Tanesco na wananchi kufanikiwa kuzima moto huo, hakuna kitu kilichookolewa katika nyumba hiyo yenye vyumba vitatu.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.