22 Jul 2005 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Akinamama Sinza B waanzisha jumuiya ya kujikomboa
 
2005-07-22 15:11:51
Na Margareth Simba, Sinza

Ili kupambana na umasikini na dhana potofu kuwa wanawake siku zote ni tegemezi, akinamama wa Sinza B, wameanzisha jumuiya yao ambayo itakuwa ikifanya shughuli mbalimbali za maendeleo ili kujiongezea kipato.

Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Bi.Imelda Limbanga amesema jumuiya hiyo inaundwa na akinamama wa Sinza B ambao wana ari ya kupata maendeleo.

’’Mpaka sasa tuko zaidi ya akinamama 40, ambao tunakutana kila baada ya kipindi maalum ili kupanga mikakati yetu, pia tumeweza kupata banda ambalo tumemkodisha mtu anayefanya biashara ya mkaa,’’akasema.

Ameongeza kuwa banda hilo huwaingizia pesa kila mwezi ambayo huwekwa kwenye akaunti ya jumuiya hiyo.

Amesema wanaangalia jinsi ya kuanzisha biashara nyingine inayolipa kutokana na pesa hizo walizokusanya.

’’Sasa hivi lazima akinamama tuwe mbele kwa kila kitu... tutakapokuwa na pato letu wenyewe tutaacha kuwasumbua waume zetu na tutajenga familia kwa kusaidiana,’’ akasema.

Aidha Bi.Limbanga amesema mbali na banda la mkaa, akinamama hao pia wamefanikiwa kujenga banda jingine ambalo wanakusudia kulitumia kufanyia biashara ya vinywaji baridi.

Naye Bi Anna Simba, ambaye ni katibu wa jumuiya hiyo amesema msaada wa kukarabati banda la vinywaji baridi waliupata toka kwa Waziri wa Chakula na Kilimo, ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ubungo, Bw. Charles Keenja.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.