|
Spika apigiwa debe
2005-07-26 15:51:40
Na Mwinyi Sadallah, Kikwajuni
Naibu Waziri wa Kilimo Zanzibar Bwana Tafana Kassim Mzee amempigia debe kubwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Bwana Pandu Ameir Kificho kwamba achaguliwe tena kushika nafasi hiyo.
Akichangia bajeti ya Wizara yake kwa mwaka 2005/06 katika Baraza la Wawakilishi, anasema Spika Kificho ameonyesha uwezo mkubwa wa kumudu kazi zake na anahisi kuna haja ya kuendelea kushika wadhifa huo.
Sioni sababu ya kumchagua spika mwingine zaidi ya Bw. Kificho, akasema na kusisitiza kwamba wawakilishi wapya watakaokuja baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 30, waendelee kumtumia spika Kificho.
Akasema mvi alizonazo Bw. Kificho ni ishara ya hekima na busara alizonazo na ana matumiani makubwa wajumbe wapya watazingatia umuhimu wa kumtumia
Bw. Kificho kuongoza baraza hilo.
Akasema ana matumaini kwamba wajumbe wote wa CCM watarudi tena katika uchaguzi ujao lakini idadi ya waujmbe wa CUF itaendelea kupungua mno.
Hata hivyo, wakati Naibu Waziri akisema hayo kwamba wajumbe wote wa CCM watarudi tena katika uchaguzi ujao lakini idadi ya waujmbe wa CUF itaendelea kupungua mno.
Hata hivyo, wakati Naibu Waziri akisema hayo baadhi ya wajumbe wa kambi ya upinzani, CUF wakiongozwa na Bw. Abubakari Khamis Bakari walikuwa wamekaa kwa utulivu mkubwa kati yao wakitingisha vichwa.
Kwa upande wake, Bw. Kificho alikuwa akimsikiliza kwa makini Bw. Tafana alipokuwa akiwashawishi wajumbe wenzake na alikaa kimya wala hakumkatiza mjumbe huyo kumpigia debe.
Bw Kificho ni Spika wa kwanza kuliongoza Baraza la Wawakilishi chini ya mfumo wa vyama vingi ambao ulianzisha Tanzania mwaka 1992.
Alichuguliwa kuwa Spika wa Baraza hilo kuanzia mwaka 1995 hadi 2000 na baadaye kuchaguliwa tena kushika wadhifa huo kuanzia 2000 hadi 2005.
Akichangia kuhusu wizara yake, Naibu Waziri huyo akasema kwamba vitendo vya wizi wa mifugo vimeongezeka kwa kasi kubwa Zanzibar na kusababisha baadhi ya wafugaji kulala na mifugo yao ndani ya nyumba zao.
|