|
Mtoto aibwa
2005-09-22 16:45:12
Na Daniel Mkate, Mikocheni
 |
 |
 |
 |
 |
 |
| |
Neema Mussa, 18, akiwa na na mtoto Nasri `Nachu` anayedaiwa kutoroka naye |
|
 |
|
|
Neema Mussa, 18, ambaye alikuwa akifanya kazi za ndani kwa Bwana Hanifu Ismail wa Mtaa wa Matumbi B Jangwani Jijini, amedaiwa kutoweka nyumbani pamoja na mtoto wa mwajiri wake mwenye umri wa miaka miwili na nusu, Nasrini Nachu .
Wazazi wa mtoto huyo Bwana hanifu Ismail na Halima Shaibu ambao walikuwa wakizungumza kwa uchungu mkubwa wamesema Neema ametoweka jana jioni akiwa na mtoto Nasrini Nachu bila kujulikana alikokwenda hivyo kuwapa wasiwasi wazazi wa mtoto huyo.
Hatukulala kabisa kwa sababu hatujui mtoto kapelekwa wapi, anakula nini, yuko hai ama vipi ndio maana tumeona tukimbilie katika vyombo vya habari, wakasema.
Baba wa mtoto huyo aliyepotea amesema Neema ambaye ni msukuma anadaiwa pia kuwa ni mwenyeji wa mkoani Dodoma.
Amesema msichana huyo wa kazi ametoweka katika mazingira ya kutatanisha kwani hakuna mtu ama jirani aliyemuona akitoroka.
Bwana Ismail ambaye amefika katika ofisi za gazeti hili mapema leo asubuhi amesema, kabla ya tukio hilo la kutoweka na mtoto, juzi kulitokea upotevu wa kiasi cha sh. 40,000, lakini kila aliyeulizwa alikana kuhusika na tukio hilo.
Akasema baada ya siku hiyo kupita bila kuelewa aliyechukua pesa hizo, jana saa 12 jioni, Neema akamchukua mtoto Nachu bila kuaga na kutoweka mpaka sasa.
Hatuelewi ameenda wapi, hivyo tunaomba msaada kwa watu ambao wataweza kumuona msichana huyo akiwa na mtoto mwenye asili ya kiasia atujulishe au apeleke kituo chochote cha polisi taarifa zake, amesema.
Amesema baada ya kuhangaika huku na huko, ametoa taarifa kituo cha polisi Msimbazi na kuandikia RB namba MS/RB/12020/2005.
Bwana Ismail amesema mtu yeyote mwenye taarifa anaweza kuwasiliana kwa simu namba 0745 678467 (Hanifu) au 0744 771775 (Hadija) ama kituo chochote cha polisi kilicho jirani.
|