Swahilinews |
 |
NAVIGATION |
 |
|
 |
|
|
 |
SEARCH |
 |
|
|
|
 |
SPECIAL |
|
|
 |
|
|
 |
ARCHIVES |
|
|
 |
|
|
 |
|
 |
|
|
|
Ranchi ya Ruvu yatoa kilio chake kwa Serikali
2005-09-26 17:11:21
Na Moris Lyimo na Haruni Sanchawa, Ruvu
 |
 |
 |
 |
 |
 |
| |
Ng'ombe wakiwa katika ranchi |
|
 |
|
|
Bei kubwa za madawa ya mifugo zimekuwa kikwazo kikubwa cha uendeshaji wa huduma ya ufugaji katika ranchi za Taifa (NARCO) na kusababisha kusuasua kwa shughuli hizo.
Meneja wa Narco wa ranchi ya Ruvu Dk.James Elirehema Mtae amesema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari waliotembelea ranchi hiyo kuona maendeleo ya sekta hiyo.
Amesema bei za madawa hayo ni kubwa mno ukilinganisha na gharama za uendeshaji, hali ambayo inabidi kutumia maarifa katika shughuli ya uendeshaji wa ranchi.
Akitoa mfano, akasema CC 1,000 za dawa aina ya BAYTICOL huuzwa hadi shilingi 77,000 kwa sasa kutoka 60,000/- za awali kwa ujazo wa lita moja, bei ambayo haiendani na gharama za uzalishaji.
Kutokana na hali hiyo, Dk.Mtae ameshauri Serikali kutoa ruzuku kwa madawa ya mifugo ili kuuzwa kwa bei ambayo inaoana na gharama nyingine ambapo kila mfugaji ataweza kumudu kununua.
Baada ya ruzuku kutengwa, tungejengewa duka maalumu ambapo tutakwenda kununua hapo. Kwa mfumo huo kiwango cha uzalishaji nyama bora kitaongezeka zaidi pamoja na mtaji kwa maana ya ongezeko la ngombe,akasema.
Akasema kwa sasa ranchi yake ina ngombe zaidi ya 3,000 na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka hadi kufikia ngombe 10,000 ifikapo mwaka 2010.
kutokana na ranchi kujiendesha kwa faida.
Pia Dk.Mtae ameelezea kusikitishwa kwake na wananchi wasioitakia mema ranchi hiyo na taifa kwa ujumla kutokana na tabia ya uchomaji moto na kuunguza majani ambayo ni chakula kikuu cha ngombe.
Akasema licha ya ranchi kusaidia kutoa ajira ndogo ndogo, misaada kwa wanavijiji wanaozunguka ranchi, baadhi yao wamekuwa wakichoma moto kwa maksudi na kuwasingizia makosa askari wao wanaolinda ranchi.
Kutokana na ukosefu wa magari, akasema ranchi inalazimika kutumia farasi kwenda kuzima moto, kuokoa ngombe wanaojeruhiwa kwa makusudi na wanavijiji wenye nia mbaya, Kibarua kingine kinachowakabili amesema ni kufukuza wafugaji wa Kimasai wanaovamia usiku na kulisha ngombe wao ndani ya ranchi.
Naye Kaimu Meneja wa ranchi, Bi.Fitina Hoza na Afisa Mafunzo Bw.Mkude Msumi wamewashauri wanavijiji kujenga mahusiano mema na ranchi kwa kuwa nia ni kuwa nao karibu kwa ajili ya kuwasadia.
Tunaomba waichukulie ranchi hii kama mali yao. Watakapoilinda ranchi na kuitetea hatimaye uchumi wa ranchi kukua, ni dhahiri kwamba itakuwa faraja kwao kwani watapata ajira pamoja na kusaidiwa zaidi huduma kama maji, na misaada midogo midogo wakati wakiwa na sherehe,akasema mama Hoza.
Kwa upande mwingine Bw.Mkude ameshauri shirika la DAWASCO kufuta mgao wa maji katika ranchi hiyo kwani shughuli za kila siku za uchinjaji zinahitaji maji.
Akasema pamoja na uchinjaji, pia matumizi ya maji kwa ajili ya kunywesha mifugo ni ya lazima lakini kutokana na ukosefu wa maji, wanalazimika kuwanywesha ngombe katika mto Ruvu ambapo ni hatari kutokana na mamba.
Maji yaliyopo hayatoshelezi kwa matumizi ya ngombe na wafanyakazi. Tunaomba mgao wa maji kwetu ufutwe kwani kwa kufanya hivyo kutaondoa kusuasua kwa shughuli zetu, akasema Bw.Mkude.
Kwa mujibu wa Dk.Mtae amesema ranchi ya Ruvu yenye ukubwa wa kilometa 43,000 ipo sehemu kubwa ya wilaya ya Bagamoyo na sehemu kidogo ya wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani na ilianzishwa mwaka 1957 ikiwa na mtaji wa ngombe sita. Kwa sasa ina ngombe 3,000.
|
|
 |
Habari za Leo |
|
|
----------------------------------------------- |
Maoni ya Mhariri |
|
|
----------------------------------------------- |
Business
bits |
|
|
----------------------------------------------- |
Makala |
|
|
| |
 |
|