Swahilinews |
 |
NAVIGATION |
 |
|
 |
|
|
 |
SEARCH |
 |
|
|
|
 |
SPECIAL |
|
|
 |
|
|
 |
ARCHIVES |
|
|
 |
|
|
 |
|
 |
|
|
|
Serikali kuandaa orodha ya wanunuzi wa mazao
2005-09-27 14:01:26
Na Mwandishi Wetu
Serikali kupitia Wizara ya Ushirika na Masoko inaandaa utaratibu wa kuwa na kitabu cha orodha ya wanunuzi wa mazao mbalimbali ili kuwasaidia wakulima kujua mfanyabiashara gani yuko wapi na anajihusisha na ununuzi wa mazao ya aina gani.
Hatua hiyo imeelezwa kuwa itasaidia wakulima kuwa na uwezo wa kuwasiliana moja kwa moja na mfanyabiashara huyo na hivyo kuondoa kero ya madalali.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Masoko katika Wizara hiyo Bw. Josephat Kriwaggulu alipowasilisha mada kuhusu jukumu la Wizara ya Ushirika na Masoko katika kutoa habari za masoko ya mazao mbalimbali yanayolimwa nchini wakati wa warsha ya wakulima na wadau wa zao la vitunguu mkoani Singida.
Alisema ukosefu wa taarifa za masoko na woga ni miongoni mwa sababu zinazowafanya wakulima wa hapa nchini wasiwe na uwezo wa kulifikia soko moja kwa moja.
Alisema ni lazima wakulima wa hapa nchini waamke na kuanza kutafuta soko wao wenyewe kwa kuwa hivi sasa wakulima kutoka Kenya na Uganda wamelichangamkia na hivyo akawataka wakulima wa nchini kupeleka mazao yao nje kuuza wao wenyewe.
Alisema wakulima nchini wamekuwa waoga kutafuta masoko wenyewe na badala yake wanatumia watu wa kati ambao hujulikana kama madalali, kitendo kinachowaumiza kwa vile madalali hao hununua mazao yao kwa bei ndogo kutoka kwa wakulima na kuyauza kwa bei ya juu ili wapate faida.
Alisema ili wakulika wafanikiwe kuondokana na umaskini ni lazima walifikie soko la mazao wao wenyewe badala ya kusubiri madalali.
|
|
 |
Habari za Leo |
|
|
----------------------------------------------- |
Maoni ya Mhariri |
|
|
----------------------------------------------- |
Business
bits |
|
|
----------------------------------------------- |
Makala |
|
|
| |
 |
|