|
Watoto wawili wagongwa na magari
2005-09-27 14:04:57
Na Mwanaidi Swedi, Polisi
Watu wawili wamekufa katika matukio mawili tofauti likiwemo la watoto wawili kugongwa na mwingine kufa.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alfred Tibaigana amesema tukio la kwanza limetokea huko Mbagala kwa Mangaya kwenye barabara ya vumbi nje kidogo na Jiji.
Kamanda Tibaigana amesema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 3:00 asubuhi ambapo gari lenye namba za usajili T514AHS aina ya Isuzu Kenta lililowagonga watoto hao wawili waliokuwa wamekaa pembeni mwa barabara na mmoja kufa hapo hapo.
Kamanda Tibaigana amewataja waliokumbwa na tukio hilo kuwa ni Salha Bakari, 6 na Habiba Idd, 5.
Aidha amesema kuwa kati ya watoto hao wawili, mmoja alikufa hapo hapo.
Mtoto huyo alimtaja kwa jina la Salha Bakari.
Kamanda Tibaigana amesema dereva aliyesababisha tukio hilo alikimbia mara ya kutokea kwa ajali.
Amesema majeruhi Habiba Idd, yuko Hospitali ya Temeke kwa matibabu na mwili wa marehemu Bakari umehifadhiwa katika Hospitali ya Muhimbili.
Katika tukio la pili mtu mmoja, Hassani Musa,25, amekutwa amekufa chumbani kwake.
Kamanda Tibaigana amesema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 1.00 asubuhi huko Magomeni Makuti mtaa wa Njombe Jijini Dar es Salaam ambapo mtu
Aidha amesema kwa mujibu wa ndugu wa marehemu Bi. Rehema Ally, chanzo cha kifo cha marehemu kilitokana na kuywa pombe aina ya gongo kupita kiasi.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Wakati huohuo, mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja ameopolewa kutoka katika choo na kufanikiwa kunusuru maisha yake.
Kamanda amesema tukio hilo lilitokea huko Makongo Juu Jijini Dar es Salaam juzi majira ya saa 3.00 asubuhi.
|