27 Sep 2005 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

CCM wachapana makonde, rungu
 
2005-09-27 14:06:15
Na Renatus Masuguliko-PST, Geita

Watu kadhaa  wakiwemo wanawake wamejeruhiwa na gari la mgombea kuharibiwa kufuatia wanachama wa  chama cha mapinduzi katika jimbo la Busanda wilayani hapa kutwangana makonde na marungu  wakigombea picha za Mgombea Urais  na Ubunge wa jimbo hilo  kupitia CCM wakidai kutopewa picha hizo ni kuwabagua kushiriki kuipigia debe CCM .

Akithibitubia jana kuwepo kwa tukio hilo kwa waandishi wa habari Mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, Bwana Faustine Kabuzi ameiambia PST kuwa  tukio hilo limetokea katika kata ya katoro jimboni humo wakatia akiwa safarini kwenda kwenye mikutanio ya kamapeni.

 ’’Ghafla nilipigwa stop na kisha wananchi hao ambao wote wanaiunga mkono CCM walizingira gari nililokuwemo  na kuanza kubandua picha za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Bwana Jakaya Mrisho Kikwete na zile zangu na kudai wanataka picha zaidi ili kushiriki katika uhamasishaji’’ amedai Kabuzi.

 Mgombea huyo akaongeza kuwa ni katika tafrani hiyo ndipo wana CCM hao walipoanza kutwangana makonde wakigombea picha hizo kwa kupokonyana na hata zile chache zilizokuwemo ndani ya gari langu walizichukua na kutioweka nazo wakati yeye akishughuklikia kuwapeleka kupata huduma ya kwanza waliojeruhiwa katika sakata hilo.

 Baadhi ya wana CCM hao  walipohojiwa kuhusiana na tukio hilo wamedai kuwa  hakuna haja kwa wagombea hao wa Urais na Mbunge huyo kuendelea kupiga debe wakati wao wapo na bado wanaamini wataibuka na ushindi wa kishindo kwa vile wanakubalika vinginevyo hata mabango ya picha zao yangetiwa moto na kuchanwa chanwa kama inavyofanyika maeneo mengine wagombea kupitia CCM wasikokubalika.

 Mgombea huyo wa Ubunge Bwana Kabuzi kupitia CCM anawania kiti hicho kwa mara ya pili mfululizo na aliteuliwa na chama hicho baada ya kuibuka na ushindi wa kishindo kwenye kura za maoni dhidi ya wapinzani wake wawili wakiambuliwa kura 34 kwa pamoja kati yakura 542 ya zilizopigwa hatua liiyaoashiria kukubalika kwake toka mwanzo.

 Akielezea adha hiyo  Bwana Kabuzi amdai tayraia ameagiza maelfu ya picha za mgombea Uraisa na zake ili kukidhi matakwa ya wananchi hao kwa vile anakiri kuwa hiyo ni ishara njema kwake na kwa mgombea Urais kuwa kataika jimbo hilo wataibuka na ushindi wa kishindo ikilinganishwa na maeneo mengine amabako picha za wagombea zimekuwa zianachanwa chanwa.

Kufuatia tukio hilo Bwana Kabuzi amedaiwa kusitisha kwa muda kampeni yake ili kushughulikia suala la upatikanaji wa picha husika,na katika mikutano yake ya kampeni amekuwa akimnadi mgombea Urais Bwana Kikwete kwa kuwaambia kuwa wampende Kikwete kama wanavyompenda yeye na kuwa wakimchagua yeye pia wampe kura Kikwete.

 Anadai kuwa wananchi wanafahamu ujasiri wake na uadilifu wake kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita walipomwajiri kuwawakilisha Bungeni toka mwaka 2000 na kama mapungufu yake pia wanayafahamu hivyo wao ndio wenye kauli ya mwisho kumtuma tena kuwawakilisha kwa kumpa kura za ndiyo.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.