|
Walokole wakwamisha Black Power
2006-07-10 14:22:59
By Adam Fungamwango, Mwananyamala
Walokole wanaoendesha ibada na maombi katika uwanja wa CCM-Mwinjuma, wamesababisha kushindwa kuchezwa kwa mechi ya soka kati ya Black Power na Bize FC za eneo hilo.
Timu hizo zilikuwa zicheze kirafiki uwanjani hapo, lakini zikashindwa kufanya hivyo kutokana na kuwepo kwa mwendelezo wa ibada ya maombi ambayo yamevuta umati mkubwa wa watu.
Viongozi wa timu hizo mbili wamesema kuwa kutokana na hali hiyo wameamua kuahirisha mechi yao hadi mkutano huo utakapomalizika.
Hatuchukii kwa sababu wanachofanya ni mambo ya Mungu na sisi wote tunamtukuza Mungu kwa hiyo kwanza ni yeye na sisi Binadamu tunafuata, ila tunataka kumwambia kuwa Mkutano huo umesababisha kuvunjika kwa pambano letu, alisema Abdallah Motego Katibu wa timu ya Black Power.
Viongozi hao wamesema kuwa mkutano huo utakapomalizika hata kama baada ya mwezi mmoja, watakutana tena na kupanga ni lini wacheze, kwani hawataki kubadilisha uwanja na badala yake wanataka kucheza kwenye uwanja huo huo ili washangiliwe na mashabiki wao ambao hujazana kwenye uwanja huo wanapocheza.
|