|
Tabata Bima Veterans vidume saba7
2006-07-10 14:23:33
By Daniel Mkate, Urafiki
Katika kusherehekea siku ya sabasaba, timu ya soka ya wazee wa Tabata Bima, juzi imefanikiwa kuwa kidedea wa bonanza maalum la soka baada ya kuichapa Survey ya Sinza kwa mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa uwanja wa Urafiki.
Katika bonanza hilo maalum la sabasaba, jumla ya timu sita zilishiriki na kuhudhuriwa na mwenyekiti wa SUMATRA David Mwaibula ambaye aliwakabidhi zawadi washindi.
Tamasha hilo lililoandaliwa na klabu ya michezo ya Friends Veterans, Kinesi Bulls na Kili Time, limewashirikisha baadhi ya wachezaji wakongwe nchini.
Safari ya Tabata Veterans kutwaa ubingwa ilianza baada ya kuwanyuka wazee Friends na kisha kukutana na Survey waliowaondoa Ukonga veterans katika mchezo mwingine wa nusu fainali.
Mmoja wa waratibu wa tamasha hilo, Michael Burton, amesema washindi wamekabidhiwa zawadi mbalimbali kutoka kwa waandaaji wake.
Naye mgeni rasmi Mwaibula amesema, michezo ya bonanza ni moja ya mbinu ya kukutanisha wachezaji na kujenga urafiki tofauti na wengine wanavyopania kuweka chuki.
Michezo ni burudani, hasa kama hapa tunavyoona wachezaji wanakunywa bia uwanjani, lakini hakuna ugomvi unaotokea, lakini sheria za michezo haziruhusu hivyo kuweka chupa za vioo uwanjani duniani kote, amesema.
|