|
8 tayari robo fainali Booster Cup
2006-07-11 14:54:25
By Abdul Mitumba, Mwananyamala
Timu nane za soka zimefanikiwa kuingia robo fainali ya kombe la Booster Rangers na kuanza kutimua vumbi Julai 13 katika uwanja wa Shule ya Msingi Mwananyamala.
Mratibu wa michuano hiyo, Abbas Ngau amesema ratiba ya hatua ya robo fainali inatarajiwa kutoka kesho.
Ngau amezitaja timu hizo ni pamoja na Linea Messina ya Magomeni, Sokoine, Depo FC za Mwananyamala, Mkunguni na Dar Stars za Ilala, Bongo Beach na Sifa United zote za Manzese na Shellys ya Kipawa.
Ameongeza katika hatua ya robo timu zitacheza mfumo wa nyumbani na ugenini na kupatikana nne ambazo zitaingia katika kinyang\anyiro cha nusu fainali.
Ngau amesema hatua ya pili ya patashika ya michuano hiyo imemalizika mwishoni mwa wiki na kutoa wiki moja kwa timu hizo kufanya maandalizi.
|