28 Aug 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wauza nyanya walilia masoko ya nje
 
2006-08-28 17:34:06
Na Margareth Simba, Temeke

  Mfanyabiashara wa nyanya akiandaa nyanya kwa ajili ya kupeleka sokoni.  
   
Wafanyabishara wa nyanya Jijini,wameililia Serikali wakiomba iwatafutie soko la nje la kuuzia nyanya kwa kuwa hivi sasa nyanya ziko za kumwaga lakini wanunuzi wachache.

Wakizungumza na Alasiri kwa nyakati tofauti, wafanyabiashara katika soko la Temeke Sterio wamesema tatizo hilo limewafanya wauze nyanya kwa bei ya kutupa na hivyo kuwapa hasara kubwa.

’’Tunaomba Serikali itusaidie ili kupata soko la nje, kwa sasa nyanya ni nyingi mno na walaji ni wachache,’’ akasema Bw. Said Mchambwa.

Mchuuzi mwingine amesema kwa sasa tenga moja la nyanya hupatikana kwa Sh. 15,000 hadi Sh 14,000 wakati hapo awali tenga moja lilikuwa likiuzwa kwa kati ya Sh. 50,000 hadi 40 kwa bei ya chini.

Mfanyabiashara mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Bi. Zakhia Omary, amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuboresha soko la nje ili kuimarisha pato la wafanyabiashara na taifa kwa ujumla pamoja na wakulima.

’’Nyanya zitaendelea kuwa nyingi mpaka mwezi wa tisa na wakulima wanasema hii inatokana na hali ya hewa kuwa nzuri,’’akasema Zakhia.

Amesema kwa hali ilivyo sasa, muda si mrefu watakata mtaji kutokana tatizo hilo.

’’Unanunua tenga la nyanya ukiamini utapata wanunuzi...matokeo yake unauza nusu na nusu zinaoza,’’ akasema mchuuzi mwingine.

Kwa mujibu wa wachuuzi hao, nyanya kibao hutoka katika mikoa ya Iringa, Mbeya na Morogoro, na husambaza katika baadhi ya masoko mbalimbali ndani ya Jiji la Dar es Salaam.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.