06 Oct 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Lowassa kuzungumzia uwekezaji Ruvuma leo
 
2006-10-06 16:39:18
Na Emmanuel Lengwa, Jijini

Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa leo anafungua mkutano wa siku moja wa uwekezaji unaofanyika mkoani Ruvuma.

Taarifa iliyotolewa Jijini na Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Lowasa tayari ameshawasili Mkoani Ruvuma kwa ajili ya mkutano huo.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Waziri Mkuu leo atafika katika Chuo cha Ualimu Songea saa 3.00 asubuhi na kufungua rasmi mkutano huo.

Taarifa hiyo inasema kuwa mada zitakazojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na Fursa za Uwekezaji mkoani Ruvuma itakayowasilishwa na Dk. Damas Mbogoro, Nmna ya kumuwezesha Mwekezaji itakayotolewa na mwakilishi kutoka kituo cha uwekezaji nchini,TIC na mikakati ya Serikali ya kuboresha miundombinu ya mkoa wa Ruvuma itakayowasilishwa na Mhandisi O. Raiser.

Mada nyingine zitakazowasilishwa ni Fursa za Uwekezaji Maeneo ya Ukanda wa Mtwara, Mitaji kwa ajili ya Wawekezaji wa Ndani na kuwakopesha Wawekezaji na Uzoefu wa Kuwekeza katika Mkoa wa Ruvuma.

Mkutano huo wa siku moja unatarajiwa kufungwa saa 10:00 jioni na Mkuu wa Mkoa huo Bi. Monica Mbega.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.