Swahilinews |
 |
NAVIGATION |
 |
|
 |
|
|
 |
SEARCH |
 |
|
|
|
 |
SPECIAL |
|
|
 |
|
|
 |
ARCHIVES |
|
|
 |
|
|
 |
|
 |
|
|
|
Kifo cha utata
2006-10-06 16:42:08
Na Selemani Mpochi, Leaders Club
 |
 |
 |
 |
 |
 |
| |
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Bw. Reginald Mengi akitoa heshima zake za mwisho mbele ya miili ya Walter Mazula na Bi. Vonetha Nkya katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam jana. Marehemu wote wawili waliuawa nchini Marekani na watu ambao hawajajulikana. |
|
 |
|
|
Ingawa ni vigumu kufahamu kilicho moyoni mwa mwenzako, lakini jana ilikuwa ni rahisi kubaini maswali kibao yaliyotanda mioyoni mwa mamia kwa mamia ya waombolezaji waliofika kuaga miili ya wachumba waliofia huko nchini Marekani.
Ni kwa nini vijana hao wameuawa?, Ni nani hasa kawaua? Utata mkubwa bado umezunguka vifo hivyo.
Huzuni kubwa ilitanda kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jana wakati miili ya Walter Mazula na mchumba wake Vonetha Nkya, vijana waliofia nchini Marekani ilipowasili hapo na kuanza kwa shughuli za kuwaaga kabla ya mazishi yao yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni.
Umati mkubwa wa watu ukioongozwa na Waziri Mkuu Bwana Edward Lowassa, mke wa Rais Mama Salma Kikwete, mawaziri wengine wa Serikali, wafanyabiashara maarufu na viongozi mbalimbali wa kidini ulikumbwa na simanzi zaidi wakati taarifa za utata juu ya kifo cha wapendanao hao zilipoanza kusomwa.
Wengi walipigwa bumbuazi kuhusiana na historia ya marehemu hao waliopendana na kukaribia kuwa mwili mmoja, na wengi wakajawa na huzuni zaidi na hisia kali za simanzi wakati Kapeteni George Mazula, baba mzazi wa marehemu Walter alipokuwa akisoma taarifa fupi kuhusiana na wapendwa wao hao.
Kwanza, ilibainika kwa waombolezaji wengi waliofurika kwenye viwanja hivyo kuwa Walter na Vonetha walikuwa na maajabu ya kufanana kwa matukio yao.
Wote walizaliwa mwaka 1979. Na wote wakazaliwa mwezi Machi ambapo aliyeanza alikuwa marehemu Walter aliyezaliwa tarehe 5, kisha wiki moja baadaye ambayo ni Machi 12, mchumba wake Vonetha naye akazaliwa.
Hiyo haitoshi, wawili hao wakarejea kwa Mungu Muumba siku moja, katika tukio moja na wana familia wa pande zote waliamua kuwafanyia mazishi ya pamoja katika siku moja, kwenye eneo moja la Makaburi ya Kinondoni jijini Dar.
Kwa mujibu wa Kapteni Mazula, utata wa kifo chao uliowafanya waombolezaji wengi wajawe na huzuni ni kama ifuatavyo:Siku ya kufariki kwao, Walter alimpitia mchumba wake Vonetha nyumbani kwake ili ampeleke kazini.
Lakini kabla ya hapo alikuwa ampitishe saluni ili kwanza akaseti nywele zake.
Matatizo yakaanzia hapo. Kamwe taarifa hazibainishi kama safari hiyo ya saluni iliwezekana ama vinginevyo.
Kufika saa 9:00 alasiri, marehemu Bi.Vonetha alikuwa bado hajafika kazini kwake. Mfanyakazi mwenzie mmoja akaamua kumsaka simuni.
Kwa bahati, simu ikapokelewa. Lakini cha ajabu ni kwamba sauti ya kike iliyojibu simu hiyo ilibainisha kuwa simu hiyo si ya marehemu Vonetha bali ni ya huyo aliyeipokea. Utata ukazidi.
Baadaye mfanyakazi huyo akaamua kumtafuta Walter kupitia simu yake.
Hii ikazidisha utata tena kwa sababu kamwe haikupatikana.
Maskini wee. Swahiba huyo wa marehemu Vonetha akaamua kumpigia kaka wa Walter aitwaye Brian Mazula na kumuarifu juu ya kutopatikana simuni kwa wachumba Vonetha na Walter.
Naye Bw. Brian alipojaribu kuwasiliana nao, akaambulia patupu.
Jitihada za kuwasaka zikaendelea. Iliposhidikana kupata taarifa zao, Brian akalazimika kutoa taarifa kituo cha polisi katika jioni ya siku hiyo juu ya kutoweka kwa wachumba hao.
Baadaye usiku, Brian akapigiwa simu na Polisi kuwa aende akautambue mwili wa marehemu Walter uliookotwa ukiwa na majeraha ya risasi.
Hiyo haitoshi, kesho yake ilikuja taarifa kuwa kuna gari lilikuwa linaungua.
Kumbe ikabainika kuwa ndani ya gari hilo alikuwepo marehemu Vonetha. Hakukuwa na maelezo zaidi na vyombio vya usalama nchini Marekani vingali vikiendelea na uchunguzi wa vifo vya wote wawili ili kuwabaini wauaji na kuwafikisha mbele ya mkono wa sheria.
Mbali na maelezo yaliyotolewa na Kapten Mazula, kulikuwa na sala za kuwaombea marehemu hao iliyokuwa ikiongozwa na Mchungaji Ezekiel Mwakisu wa Kanisa la Kilutheri Mbezi.
Kisha zikatolewa salamu za rambirambi kutoka kwa Watanzania wanaoishi Marekani zilizosomwa na mwakilishi wao Bi. Mercy Muro ambaye pia alikabidhi mchango wa dola za Kimarekani 36,000 ikiwa ni rambirambi kwa marehemu hao.
Kisha baada ya kukamilika kwa shughuli zote kwenye viwanja hivyo, ambavyo vilipambwa kwa nyimbo za maombolezo toka kwa wana kwaya mbalimbali, majeneza yaliyokuwa na miili ya marehemu hao yalitolewa toka kwenye kibanda maalum kilichopambwa kwa maua na msafara wa kuelekea makaburi ya Kinondoni ukaanza.
Wazazi wa pande zote mbili walikuwa mstari wa mbele katika kuongoza mazishi hayo, huku wote wakiwa katika mavazi ya rangi nyeusi na wale wa kike wakiwa na ziada ya kofia nyeusi.
Nimempoteza mtu muhimu... Walter si kwamba alikuwa mwanangu tu, bali pia alikuwa ni rafiki yangu wa karibu, alisema Kapteni Mazula kabla ya msafara wa kuelekea makaburini Kinondoni.
|
|
 |
Habari za Leo |
|
|
----------------------------------------------- |
Maoni ya Mhariri |
|
|
----------------------------------------------- |
Business
bits |
|
|
----------------------------------------------- |
Makala |
|
|
| |
 |
|