18 Oct 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

PPT - Maendeleo waichimba mkwara Tanesco
 
2006-10-18 18:06:55
Na Sharon Sauwa, Mikocheni

Chama cha PPT Maendeleo kimempa siku tatu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini, Tanesco kueleza umma juu ya kile kinachoendelea ndani ya shirika lake.

Aidha, chama hicho kimemtaka Mwenyekiti huyo atoe maelezo kwa Watanzania kuhusiana na mkataba wa utata wa shirika hilo na kampuni ya Richmond ya Marekani ambayo imepewa kazi ya kuingiza jenereta za kuzalishia umeme.

Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Peter Mziray, pamoja na mambo mengine analia na Mwenyekiti wa Tanesco akitaka aeleze ni kwa namna gani Richmond walishinda kazi kubwa kama hiyo bila kuchunguzwa uwezo wao na kuwa kama kuna Watanzania vigogo waliopo ndani ya kampuni hiyo watajwe.

’’Pia kwa hali hii ni hatua gani zinachukuliwa kupata mbadala wa Richmond. Na mwisho Watanzania tuelezwe ukweli ni lini hasa mgao wa umeme unakwisha,’’ akasema Bw. Mziray katika taarifa hiyo, bila kutaja ni hatua gani watachukua endapo Tanesco haitatekeleza agizo lao hilo.

Chama hicho kimeitaka serikali kutoona aibu kutangaza mgao wa umeme kuwa ni janga la kitaifa ili iweze kusaidiwa kwa kuwa yenyewe imeshashindwa.

Akasema Mziray kuwa itakuwa busara kwa Serikali ya CCM kukubali kwamba taarifa za kuhusiana na kampuni ya Richmond na tatizo la umeme limewashinda.

Akailamu Serikali ya TANU na CCM, kuwa haikuweza kuona mbali na kufikiria jinsi ya kutatua matatizo ya umeme huku wakijua kwamba sayansi na teknolohjia vyote vyahitaji umeme.

Hatua ya chama hicho ya kutaka ufafanuzi kuhusiana na jambo hilo, inatokana na gazeti moja linalochapishwa kila siku kuelezea habari ya kukwama kwa jenereta hizo nje ya nchi kutokana na ukosefu wa usafiri.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.