18 Oct 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Dereva wa daladala anyakua milioni kwa kunywa Coca moja
 
2006-10-18 18:08:23
Na Caroline Mosha

Mshindi wa kwanza wa promosheni ya Vuna pesa na Cocacola Bw. Boniface Steven, ambaye ni dereva wa daladala ya Kariakoo na Temeke amenyakua kitita cha Sh.milioni 1 kutoka kampuni ya Cocacola Kwanza.

Mshindi huyo alikabidhiwa fedha hizo jana na Meneja Masoko wa Kiwanda cha Cocacola Bw. Francis Nanai.

Hafla ya kuwakabidhi washindi zawadi zao ilifanyika kwenye ofisi za kiwanda hicho kilichopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam.

Bw. Nanai amesema mshindi huyo amebahatika kujishindia kiasi hicho cha fedha baada ya kunywa soda ya Cocacola juzi.

Ametaja mshindi mwingine ambaye amejinyakulia Sh. 500, 000 kuwa ni Bw. Ibrahim Toba mkazi wa Gongo la Mboto.

Bw. Nanai amewataja washindi wengine waliokabidhiwa fedha zao kuwa ni Bw. Erasto Mkweli na Bw. Nicholaus Ching’enya ambao wamejishindia Sh.50,000 kila mmoja.

Akizungumzia shindano hilo, Bw. Nanai amesema limeingia wiki ya pili na kwamba mshindi wa wiki ya kwanza wa Sh. milioni moja alikuwa Bw. Richard Manyembe.

Amesema shindano hilo linazidi kuwanufaisha wanywaji wengi wa Cocacola na Fanta kwa kujishindia zawadi mbalimbali.

Ametoa ushauri kwa Watanzania kunywa kwa wingi soda hizo ili waweze kujishindia zawadi mbalimbali.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kitita chake, mshindi wa Sh. milioni moja Bw. Stephen amewashukuru Cocacola kwa kuandaa shindano hilo.

’’Kwa kweli sikutarajia kama nitapata kiasi hiki cha fedha kwa mkupuo…nawashauri Watanzania waendelee kunywa Cocacola ili washinde kama mimi’’, amesema.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.