21 Oct 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mziray amuomba JK kibarua
 
2006-10-21 14:19:49
Na Usu-Emma Sindila, Jijini

Mwenyekiti chama cha PPT-Maendeleo Taifa Bwana Peter Mziray amemwomba rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Jakaya Kikwete kumpa kazi kwenye bodi ya wakurugenzi wa Tanesco.

Bw. Mziray amesema amefikia uamuzi huo ili aweze kuishauri bodi hiyo pamoja na mkurugenzi wake namna ya kukabiliana na tatizo la umeme nchini.

Bw. Mziray alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salam.

Alisema tatizo la umeme nchini limekuwa kero kwa nchi nzima na pia linatia kichefuchefu.

”Mimi siutaki uenyekiti, naomba wanipe japo ujumbe tu katika bodi niwe naongea tuu!...Lakini najua hawawezi kunipa kwa kuwa mie ni mpinzani,” akasema.

Amesema kutopatikana kwa umeme ni kutokana na kutokuwa na sera makini na pia kuchanganywa kwa sera mbili za serikali na za chama.

”Ilani ya chama ni njia ya kuombea kura kwa wananchi wako, ukishaingia madarakani unatakiwa kutumia sera za Serikali ambazo ndizo zenye kutekelezeka na si kwenda katika maofisi ya serikali ukiwa umebeba ilani za chama chako,” akasema.

Amesema endapo utapeleka kila kitu kwa mtindo wa kutumia sera za chama, lazima utafeli kwa kuwa hazitekelezeki.

Amesema hali ya maisha kwa sasa ni ngumu ukilinganisha na hali ya maisha ilivyokuwa kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika mwishoni mwa mwaka jana.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.