26 Oct 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Vita dhidi ya umaskini ni ya wote
 
2006-10-26 15:14:45
Na Kiyao Hoza

Vijana wanaoishi na virusi vya ukimwi, wanatazamiwa kuwa miongoni mwa washiriki wa kampeni ya kuondoa umaskini nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chama cha Vijana wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, TAYOPA, Bi. Anifa Amir amesema vijana hao watajadili kwa pamoja kuhusu upatikanaji wa huduma na matibabu kwa watu wa kundi hilo.

Pia kampeni hiyo itawakutanisha wadau mbalimbali wa masuala ya ukimwi ili kujadili kuhusu bima ya afya kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

”Vijana na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi bado wana matatizo katika bima ya afya... wanahitaji kukaa na kujadili tatizo hilo,” akasema Bi. Hanifa.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanafunzi wa Sayansi ya Siasa (Political Science) wa Chuo Kikuu Dar es salaam, DUPSA, Bi. Grace Mesh, amesema kuwa wadau wa elimu ya juu watashiriki katika kampeni hiyo kwa kutoa maoni yao juu ya mfumo wa elimu hasa kwa vyuo vikuu uliopo nchini.

”Wadau mbalimbali watazungumzia suala la elimu ya juu, kwa mfano jinsi umaskini unavyochangia wanafunzi kushindwa kujiunga na vyuo vikuu,” akasema Bi. Mesh.

Awali akizungumzia kuhusu kampeni hiyo, Mratibu wa mawasiliano wa Asasi isiyo ya kiserikali inayopambana na Umasikini, ActionAid, Bw. Albert Memba, amesema msisitizo wa kampeni hiyo unalenga kuhamasisha viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani, wabunge na serikali kuu ili kuongeza kasi ya maendeleo.

Amesema iwapo serikali itatimiza malengo ya milenia katika kuleta maendeleo ni wazi dhamira ya kuondoa umasikini itakuwa imefikiwa na hivyo kutengeneza maisha bora kwa kila Mtanzania.

Kampeni hizo zinazoendelea katika mikoa mbalimbali nchini hivi sasa, zitafikia kilele chake Oktoba 16 mwaka huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini ambapo wanaharakati watasimama na kuitaka serikali ichukue hatua za haraka dhidi ya umasikini.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.