26 Oct 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Matajiri waaswa kutoa sadaka kwa familia zisizo na uwezo
 
2006-10-26 15:16:46
Na Futuna Seleman,TEMEKE

Waislamu wenye uwezo hapa nchini wametakiwa kutoa sadaka ya zaka l-fitri kwa familia zisizo na uwezo kwa kuwapa kilo mbili na nusu za mchele ili kuweza kupata thawabu
’Kiulaini’ kutoka kwa MwenyeziMungu.

Akizungumza kabla ya swalati subuhi mmoja wa sheikh aliyekuwa akiwaamsha watu kwa njia ya kipaza sauti ili wapate kula daku na kujiandaa na swala hiyo siku tatu kabla ya kuswaliwa idd El-fitri alisema kuwa siku zimeshafika kwa waislamu kutoa sadaka hiyo.

Alisema sadaka ya zaka l-fitri hutolewa kabla ya kuswali Idd na ikitolewa baada ya hapo huesabiwa kama sadaka ya kawaida.

”Sadaka ya zaka l-fitri inaanza kumilamwisho,leo bado siku tatu wenye uwezo toeni kuanzia kilo mbili na nusu ya chakula unawapa wasio na uwezo,”.akasema Sheikh huyo.

Akasema ni vema waislamu wenye uwezo wakawanunulia wasio na uwezo mchele usio na chenga mzuri ulioonyooka.

”Kwa kufanya hivyo unawasaidia kwa kila familia isiyokuwa na uwezo na pia unawalinda wazazi wako ama nduguzo waliokwishatangulia ahera,”.akasema Sheikh.

Pamoja na mambo mengine akawataka waislamu wote kujipinda na kumaliza kufunga mwezi wote mtukufu wa ramadhani bila kukatiza hata chungu kimoja.

’Jipindeni mmalize kufunga mwezi mtukufu wa ramadhani bila kukatiza na kisha sameheaneni kwa kuombana radhi za kweli kwa mambo mabaya mliyotendeana mtapata swawabu.”

Aidha, akawataka na wale wenye uwezo wa kujinunulia chakula cha siku nzima nao wawanunulie wenzao na wale watakaobahatika kupata mgao wa chakula kingi wawagawie wenzao wasiopata kabisa.

”Nendeni Tandika dabokibini mnunue mchele ulioonyooka, wapeni wasio na uwezo. Huwezi kubeba mchele toa pesa ya mchele huo mzuri na nyie mtakaopewa kilo nyingi toeni kwa wenzenu wasiopata kabisa.”

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.