26 Oct 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Aliyesombwa na treni aendelea vizuri
 
2006-10-26 15:17:25
Na Moshi Lusonzo,Muhimbili

Yule mkazi wa Tandika aliyegongwa na treni baada ya kupandwa na hasira zilizomfanya ajilaze relini, amenusurika kukatwa mkono.

Licha ya jamaa huyo |Bw. Mfaume Selemani, 35, kunusurika kukatwa mkono bado hajaanza kupata kumbukumbu za kutosha, zaidi ya kukumbuka kitu kimoja ambacho ni pombe aliyokunywa kabla ya kugongwa na treni.

Awali Mfaume alilazwa wodi namba 17 jengo la Sewahaji, lakini kutokana na majeraha aliyoyapata ilibidi ahamishiwe katika wodi namba 18 ambayo ni maalum kwa wagonjwa wenye majeraha makubwa au wanaosubiri kupewa matibabu ya kuondolewa viungo.

Habari zilizopatikana hospitalini hapo zinaeleza kuwa mkono wake wa kulia ambao ndio uliojeruhiwa vibaya unaonekana kuanza kuimarika.

Gazeti hili lilipozungumza naye, hakuwa na kumbukumbu za tukio zima zaidi ya kukumbuka pombe kupita kiasi alizogida siku hiyo.

”Nilikunywa pombe sana, hapo tena sijui chochote kilichoendelea,” akasema.

Hata hivyo, Afisa Uhusiano wa MOI, Bw. Almas Jumaa amesema mgonjwa wao anaendelea vizuri.

Katika tukio lingine, mkazi wa Boko Geofrey Milulu,23, amelazwa katika hospitali hiyo baada ya kupigwa na watu wasiojulikana.

Katika tukio hilo, Milulu ameumia kichwani na alifikishwa hospitalini hapo majira ya saa 6:00 usiku na kuwahishwa wodini kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Mtu huyo amelazwa wodi namba 17 jengo la Sewahaji na juhudi za kumfanyia uchunguzi wa kina zinaendelea.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.