26 Oct 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Majambazi yapigwa bao
 
2006-10-26 15:22:04
Na Charles Masanyika, PST, Manyara

Majambazi yaliyokuwa katika harakati za kufanya uporaji katika benki moja mkoani hapa yamezidiwa akili na Polisi baada ya kustukiwa \’dili\’ lao hilo na kisha kuharibiwa kwa mpango wao wote.

Majambazi hayo yanadaiwa kuwa yalikuwa yamejibanza kwenye kundi la waumini wa dini ya Kiislamu na baada ya kustukiwa ndipo yaliposambaratishwa kutokana katika operesheni iliyohusisha mabomu ya machozi na risasi kadhaa za moto zilizokuwa zikipigwa hewani.

Tukio hilo la kuzidiwa akili kwa watu hao wanaodaiwa kuwa majambazi lilijiri huko eneo la Kibaya wilayani Kiteteo mkoani hapa wakati wa kufanyika kwa mhadhara wa Kiislamu uliokuwa ukiendeshwa na Mhadhiri Salum Ibrahim kutoka Jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Neven Mashayo, amekiri jeshi lake kuwatawanya waumini waliokuwa kwenye mhadhara huo kwa kutumia silaha na kueleza kuwa walilazimika kufanya hivyo kwa hofu kuwa waliokuwemo katika tukio hilo hawakuwa waumini bali mijamaa iliyokuwa kwenye windo la uvamizi wa benki.

Hata hivyo haikufafanuliwa zaidi juu ya kunyakwa kwa mijamaa hiyo iliyokuwa katika harakati za uporaji.

Tukio hilo lililowatawanya waumini wa Kiislamu waliokuwa kwenye mhadhara.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.