27 Oct 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

’Vita dhidi ya ukimwi haitaki watazamaji’
 
2006-10-27 19:22:32
Na Kiyao Hoza, Kinondoni

Imeelezwa kuwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa,vita dhidi ya ukimwi inahitaji ushirikiano kati ya viongozi na wananchi wanaowazunguka.

Wito huo umetolewa na mmoja kati ya wakala wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini, TACAIDS, Bw. Charles Lupily wakati akizungumza na viongozi wa vikundi vya kupambana na ugonjwa huo vilivyoko katika wilaya ya Kinondoni.

Amesema tatizo lililopo hivi sasa na linalokwamisha juhudi zinazofanyika katika kupunguza kasi ya maambukizi mapya ni kwamba zoezi hilo linafanywa na baadhi ya watu huku wengine wakibaki kuwa watazamaji tu.

’’Raha ya ngoma ni uingie ucheze na si kuwa mtazamaji tu, hivyo kila mmoja kati yetu anatakiwa kuwa mshiriki katika zoezi hili,’’ akasema Bw. Lupily.

Wakati huo huo Bw. Lupily amewashauri wananchi wanaoishi katika maeneo mbalimbali jijini, kujiunga na vikundi vya kupambana na ugonjwa huo vilivyoko katika maeneo yao.

Amesema hiyo ni njia mojawapo inayoweza kutumika katika kubadilishana mawazo na kupata mbinu mbadala za kujikinga na ugonjwa huo.

Pia amewataka viongozi hao kushirikisha wananchi wakati wanapoanzisha miradi mipya ili wapate maoni kutoka kwao.

”Mnapofikiria kuanzisha miradi ya kupambana na ugonjwa huu, ni muhimu kuwashirikisha wanachi na kukaa na kupanga wenyewe,” akasema.

Akasema ushirikishwaji wa wananchi unasaidia kufanikisha miradi hiyo kwa kuwa wao ndio waathirika na walengwa wa miradi hiyo.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.