01 Nov 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Pindupindu laendelea kusumbua wakazi Jijini
 
2006-11-01 16:32:17
Na Kiyao Hoza, Jijini

Gonjwa la kipindupindu bado linaendelea kusumbua wakazi Jijini Dar ambapo hadi kufikia jana, wagonjwa wapya 37 wameripotiwa na hivyo jumla ya wagonjwa wote kuwa 84 katika manispaa zote tatu.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu gonjwa hilo, Mganga Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Deo Mtasiwa, amesema taarifa zinaonyesha kuwa Jiji bado linakabiliwa na mlipuko wa ugonjwa huo katika manispaa zote za Temeke, Ilala na Kinondoni.

Akasema kati ya wagonjwa hao, 23 wanatoka katika manispaa ya Ilala, 12 wanatoka Kinondoni na wawili wanatoka Temeke.

Ameyataja maeneo wanakotoka wagojwa hao kuwa ni Kiwalani, Ukonga, Tabata, Buguruni, Vingunguti, Ubungo, Kigogo, Ilala na Segerea.

Maeneo mengine ni Mbagala Kuu, Mtoni Bustani, Mwananyamala, Msasani, Kimara, Ubungo, Mburahati na Manzese.

Dk. Mtasiwa amesema katika hospitali za manispaa zote tatu, kuna jumla ya wagonjwa 47 waliokuwa wamelazwa kabla ya mlipuko mpya wa wagonjwa 37.

Akasema kufuatia hali hiyo, zoezi la ukaguzi wa usafi katika maeneo tofauti Jijini lianendelea katika manispaa zote, likihusisha pia majengo na kwenye maeneo ya biashara.

Pia Dk. Mtasiwa amepiga marufuku tabia ya baadhi ya wananchi kutiririsha maji machafu na kutupa taka hovyo mitaani.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.