20 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Simba: Athuman Idd amechafua jina letu
 
2006-12-20 16:12:23
By Badru Kimwaga, TSJ, Msimbazi

Uongozi wa klabu ya soka ya Simba umesema hauna hofu na hatua ya kiungo wao, Athuman Idd kuamua kukimbilia Polisi kulalamikia kughushiwa saini yake.

Pamoja na hayo, uongozi huo umemshutumu mchezaji huyo kwa kulichafua jina la klabu hiyo kufuatia kauli yake kuwa viongozi walighushi ’dole gumba’ lake.

Kiungo huyo aliamua kukimbilia Polisi kutaka msaada wa kisheria akipinga kutia saini fomu za usajili za CAF za Simba, ambapo kesi yake imefunguliwa kituo kikuu cha polisi cha Jijini kwa jalada lenye namba CD/RB/14212/06 na CD/RB/5220/06.

Katibu Mwenezi wa Simba, Seydou Rubeya aliliambia Alasiri leo kuwa, wao hawapingi mchezaji huyo kwenda kutafuta sheria kwenye vyombo vinavyohusika, lakini akasisitiza kuwa viongozi wa klabu hiyo hawana utamaduni wa kughushi saini za watu.

’’Ametuchafulia jina, hatufanyi kazi katika utaratibu kama huo, yeye mwenyewe anafahamu hiyo, sasa kitu gani kingine anatafuta,’’ alisema.

’’Hatupendi kuliongelea suala hilo kwa mapana zaidi kwa vile kwa sasa liko Polisi, pia tunao mkataba wake halali,’’ alifafanua zaidi bosi huyo.

Seydou alisema kuwa wanashindwa kuelewa mchezaji huyo ana matatizo gani wakati saini ya kuingia mkataba na Simba aliiweka mwenyewe kwa hiari yake kwamba atakaa nao mpaka mwaka 2008.

Kiungo huyo anayeng’ang’ania kwenda Yanga badala ya kuichezea Simba msimu mmoja wa ligi, amekaririwa na vyombo vya habari kutinga kituo kikuu cha polisi cha jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwashtaki viongozi wa Simba kwa kile alichodai wameghushi saini yake katika usajili.

  • SOURCE: Alasiri
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.