21 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Siku 365 akiwa Rais
 
2006-12-21 16:43:44
Na Mwandishi Wetu, Jijini

Siku ya 365 tangu Rais wa awamu ya nne, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipoingia Ikulu, ameeleza yaliyo moyoni.

Katika mahojiano maalum na baadhi ya wana habari, Rais ameeleza mambo ya msingi ambayo Serikali yake imefanikiwa kuyafanya katika kipindi hicho cha mwaka mmoja.

Akasema japo ni kipindi kifupi ambacho amekaa madakani lakini anaridhika na kiasi ambacho Serikali yake imefanikiwa.

Akasema mwaka huo mmoja aliokaa Ikulu anaugawa katika vipindi viwili yaani sehemu ya kwanza ya wao kupanga nini watakachokifanya na ya pili ya kuanza utekelezaji.

’’Nakumbuka tulifanya mkutano wetu wa kwanza wa Baraza la Mawaziri. Tukaambiana kwamba kila mmoja aende kwake kupanga mpango wake wa namna ya kutekeleza majukumu yake kwa miaka mitano ijayo kwenye wizara yake,’’ akasema.

Akaongeza, ’’tulipeana miezi mitatu ya kufanya kazi hiyo. Nashukuru kwamba kazi ile ilikamilika. Na miye pia katika kipindi hicho nimezunguka kwenye wizara, kuzunguka kwenye mikoa, na kwenye idara za Serikali kwa maana ya kujifunza kujua hali halisi ikoje ili tuweze kukaa na kupanga.

Na yale ambayo tulikuwa tumeamua kupanga sasa yakawa yameingia kwenye bajeti ya kwanza Julai, mwaka huu’’.

Akasema hana wasiwasi kabisa kwamba malengo ya Serikali yake watayafikia.

’’Tunaweza kuyafikia yote kabisa ama tunaweza kufikia sehemu kubwa. Katika hotuba yangu ya Bunge nilieleza karibu mambo kumi tuliyokusudia kuyafanya.

Moja ilikuwa ni kudumisha uhuru wa nchi yetu, kudumisha amani, utulivu na umoja wa taifa letu. Katika kipindi hiki nina hakika tumefanikiwa.’’ akasema.

Akasema la pili ambalo aliwaahidi Watanzania kupambana na uhalifu, hasa ujambazi, kuhakikisha kwamba usalama wa nchi unakuwepo.

’’ Kipindi kile ulikuwa ukiamka asubuhi wamepiga hapa mara wako bureau de change hii, mara selander bridge mara wapo mtaa huu.

Mimi nadhani na ninyi mashahidi kwamba jitihada kubwa tumefanya na tumeweza kabisa kulipunguza lile wimbi la ujambazi.’’

Kadhalika Rais anasema katika kipindi hicho japo kifupi, lakini Serikali yake imefanikiwa kuongezeka jitihada za kukuza elimu nchini.

Pia akasema Serikali yake imejitahidi kuimarisha mipango ya mapambano dhidi ya umaskini na kuendelea kubuni mbinu za kukuza uchumi.

Kadhalika Rais akazungumzia vita dhidi ya kero zinazowaumiza wananchi kila kukicha ikiwa ni pamoja na suala la umeme.

Lakini pia katika mazungumzo yake, Rais Kikwete ambaye leo anatazamiwa kulihutubia taifa, akazungumzia changamoto kadhaa zilizopo katika kufikia malengo ya serikali katika kuwaletea Maisha Bora Watanzania, hivyo kwa namna nyingine kuwa sehemu ya karaha.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.