23 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Shirikisho, Kaole kukutana Kinesi kesho
 
2006-12-23 13:48:24
By Mwandishi Wetu, Jijini

Timu mbili za soka za wasanii wa maigizo nchini, Shirikisho FC na Kaole SC, zinatarajiwa kukutana tena Jumapili ijayo katika mechi ya marudio ya kombe maalum la Kinesi kwenye uwanja wa Kinesi Bulls uliopo Urafiki, Jijini.

Awali timu hizo zilipokutana katika mechi ya kwanza katika uwanja huo, zilitoka sare ya bao 1-1.

Mratibu wa michuano hiyo, Joseph Itang’are, amesema mshindi wa mechi hiyo atakuwa amevuka kikwazo cha kuingia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo itakayoshirikisha timu nane.

Naye mchezaji wa Shirikisho, Samson ’Mandieta’, amesema ana uhakika timu yake itasonga mbele iwapo waamuzi watachezesha kwa haki mchezo huo.

”Timu yetu ni nzuri isiyo na mamluki, hivyo tutacheza kitimu na kuweza kusonga mbele,” amesema ’Mandieta’.

  • SOURCE: Alasiri
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.