23 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Miss Utalii kusaka vipaji Krismas
 
2006-12-23 13:48:54
By Mwandishi Wetu, Ubungo Plaza

Jumla ya warembo 34 kutoka mikoa mbalimbali nchini, ambao watashiriki fainali ya Taifa ya Miss Utalii 2006, wataanza kinyang’anyiro cha kusaka vipaji keshokutwa katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Jijini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Rais wa Kamati ya Miss Utalii nchini, Gideon Chipungahelo, amesema katika shindano hilo, warembo wataonyesha nyimbo mbalimbali za kiasili kwa kucheza pamoja na na kuimba.

”Warembo pia watatangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika mbuga zetu mbalimbali zikiwemo Mikumi, Ngorongoro, Serengeti na Manyara,” amesema Chips.

Aidha, amesema warembo hao pia watashindana Desemba 30 kuwania taji la Miss Utali Taifa, mchuano utakaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Amesema washindi watano watakaopatikana watawakilisha nchi katika shindano la Miss Utalii Dunia huku wa kwanza akiwakilisha Miss Utalii, wapili Miss Intenati, miss milionea wa tatu, miss Bikini na miss Model.

  • SOURCE: Alasiri
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.