27 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Serikali yahimizwa kusaini Mkataba wa Haki za Walemavu
 
2006-12-27 18:38:44
Na Mwanaidi Swedi, Jijini

Serikali ya Tanzania imetakiwa kuupa kipaumbele Mkataba wa Kimataifa juu ya haki za wenye ulemavu uliopitishwa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa ili iwe miongoni mwa nchi 20 za kwanza kusaini mkataba huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la walemavu la kutetea haki za kisheria na jamii, DOLASED, Bw. Gidion Mandesi, amesema kuwa mkataba huo uliopitishwa Desemba 13, mwaka huu unalengo la kukuza na kulinda kikamilifu haki za watu wenye ulemavu kote duniani.

Aidha ametoa shukrani kwa serikali ya Tanzania pamoja na wadau wengine kama vile wawakilishi wa mashirika ya kijamii na yale ya kitaifa, kwa michango yao muhimu wakati wa majadiliano ya uundwaji wa mkataba huo.

’’Mkataba huu ni matunda ya ushirikiano wa serikali za nchi mbalimbali na vyama vya kijamii hasa vya watu wenye ulemavu na taasisi huru za haki za binadamu,’’ amesema Bw. Mandesi.

Akasema kuwa mkataba huu ni wa kwanza kutungwa na Umoja wa mataifa katika karne ya hii 21, ambao unakataza ubaguzi katika nyanja zote za maisha dhidi ya watu wenye ulemavu.

Akaongeza kuwa mkataba huo ni kielelezo kizuri kinachoonyesha ufanisi wa Umoja wa Mataifa katika kutekeleza majukumu yake.

Amesema kuwa hii haijawahi kutokea katika historia ya Umoja wa Mataifa kuandaa na kukamilisha mkataba wa haki za binadamu kwa kipindi kifupi, pamoja na kuwashirikisha wadau mbalimbali kwa ajili kuandika na kujadili mkataba wa kimataifa.

Bw. Mndesi amesema kuwa makataba huu umeweka bayana haki zote za binadamu kwa mtazamo, ustawi na maendeleo ya watu wenye ulemavu.

Mambo yaliyopewa kipaumbele katika mkataba huo ni pamoja na huduma za jamii na vifaa kwa ajili ya watu wenye ulemavu, kupinga vitendo vya unyanyasaji na ukatili kwa watu wenye ulemavu.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.