04 Jan 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Serikali yaja na dawa ya ujenzi holela Dar
 
2007-01-04 17:50:47
Na Mwanaidi Swedi, Jijini

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imebuni mpango wa kuyaendeleza maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam kabla hayajavamiwa na kusababisha ujenzi holela kama unavyoonekana katika maeneo mengine.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi.Salome Sijaona, amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa mpango huo ni wa kutenga ardhi ya kutosha kwa ajili ya huduma za jamii na miundombinu ili kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya huduma hizo kwa wakazi wa Jiji.

Aidha, amsema Bi. Sijaona kuwa Jiji limekuwa na ongezeko kubwa la wakazi ambapo sasa linakadiriwa kuwa na zaidi ya watu milioni tatu.

“Ongezeko hili la watu limeathiri uendelezaji wa Jiji kwa kiasi kikubwa na kusababisha ujenzi holela kama unavyoonekana katika maeneo mbalimbali yakiwemo Manzese, Tandale, Yombo na Tandika, “ amesema Bi. Sijaonja.

Akasema katika maeneo hayo, ujenzi ulisambaa mpaka kwenye maeneo ya hatari ambapo uendelezaji wake haukuambatana na huduma za jamii na miundombinu hali ambayo ni hatari kwa afya.

Amesema katika mpango huo baadhi ya nyumba zitatakiwa kubomolewa ili kutoa nafasi kwa uwekaji wa huduma hizo na watalipwa fidia kwa mujibu wa sheria ya Ardhi Namba 4 ya mwaka 1999.

Pia amesema maeneo yatakayohusika na mkakati huo ni Manispaa zote za Jiji la Dar es Salaam.

Bi. Sijaona amesema mpango huo ukifanikiwa, utakuwa na manufaa kwa wakazi ambao wataweza kupata huduma za kijamii karibu na hivyo kupunguza gharama za usafiri na muda unaopotea katika kufuatilia huduma hizo katikati ya Jiji.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.