16 Feb 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Moto wateketeza jumba la vyumba sita Jijini
 
2007-02-16 17:14:29
Na Usu-Emma Sindila, Jijini

Moto mkubwa umezuka pale Magomeni Mapipa Bondeni na kuteketeza nyumba ya vyumba sita na vitu vyote vilivyokuwamo.

Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Bi. Avelyne Luoga, amesema moto huo umezuka jana mishale ya saa 1:30 asubuhi.
Amesema nyumba hiyo ilikuwa mali ya Bw. Jamal Mwakasala, 30, mfanyakazi wa kampuni ya Mabasi ya SABCO.

Kamanda Luoga amesema chanzo cha moto huo ni mtoto wake wa miaka 3 ambaye alikuwa akichezea kibiriti na kusababisha godoro kushika moto na hatimaye nyumba nzima ikashika moto na kuteketea yote.

Hata hivyo, amesema thamani halisi ya mali iliyopotea haijafahamika na hakuna mtu aliyejeruhiwa.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.