21 Apr 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Kuku wa `uswazi` kupatiwa chanjo Temeke
 
2007-04-21 18:56:16
Na Futuna Seleman,Temeke

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, imetoa mafunzo kwa watu wanaotoa chanjo ya kudumu ya kuku katika kata zake 15 za manispaa hiyo.

Mafunzo hayo yanalenga kudhibiti magonjwa ya kuku wa kienyeji.

Afisa Uhusiano wa Manispaa hiyo, Bi. Alice Msumba ameliambia Alasiri kuwa kuku watakaochanjwa ni wale walioko katika kata zilizobainika kuwa na tatizo kubwa la magonjwa ya kideri na ndui ambayo huangamiza kuku kuku wengi wilayani humo.

Akasema kati ya kata 24 zilizomo katika manispaa hiyo, kata 15 zimeonekana kuwa na tatizo hilo kwa kiwango kikubwa zaidi.

Akasema kata hizo zimebainika kufuatia utafiti uliofanywa, ambao umewezesha kupata takwimu sahihi za vifo vya kuku wa kienyeji katika kila kata.

Akazitaja kata hizo kuwa ni Yombo Vituka, Chamazi, Charambe, Tuangoma, Kibada, Kisarawe 11, Vijibweni, Mbagala Kuu, Mbagala, Makangarawe, Kigamboni, Mjimwema, Somangira, Kimbiji na Pemba Mnazi.

Akasema hadi sasa, tayari kuna watu wanne waliopewa mafunzo maalum ya kuendesha zoezi hilo la kuchanja na kisha kusimamia zoezi hilo kwa wafugaji wengine.

Bi. Alice amesema katika mitaa yote ndani ya kata hizo, wananchi watatozwa gharama ya Sh. 30 kwa kila kuku, wakiwemo vifaranga.

``Tunaamini kwamba pesa kidogo zitakazopatikana, zitatumika kuendeleza shughuli ya uchanjaji na hatimaye kuweza kutokomeza kabisa vimelea vya kideri na magonjwa mengine ya kuku,`` akasema Bi. Alice.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.