21 Apr 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mfanyabiashara Jijini adakwa na kucha kibao za simba, chui
 
2007-04-21 18:58:36
Na Mwanaidi Swedi, jijini

Mfanyabishara mmoja wa vinyago Jijini amejikuta yuko matatani baada ya kukutwa na nyara kibao za serikali ikiwa ni pamoja na seti ya kucha za Simba na vifaa kedekede vilivyotengenezwa kwa meno ya tembo.

Mfanyabiashara huyo aliyetajwa kwa jina la Ruben Simkoko, 30, anadaiwa kumiliki nyara hizo za Serikali kinyume cha sheria.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Jamal Rwambo, ameliambia Alasiri kuwa aarifa za mfanyabiashara huyo kumiliki nyara za Serikali zilimfikia jana, mishale ya saa 9:30 alasiri.

Kamanda Rwambow amesema baada ya taarifa hizo wakafanya uchunguzi na kufanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo.

Kamanda Rwambow amezitaja nyara alizokamatwa nazo mtu huyo kuwa ni meno matano ya tembo, kucha 14 za chui, kucha 10 za Simba, mikufu saba iliyotengenezwa kwa kutumia mkia wa tembo, mikufu mitatu iliyotengenezwa pia kwa meno ya tembo na vinyago vitatu vya binadamu ambavyo pia, vyote enye vimetengenezwa kwa meno ya tembo.

Nyara nyingine ni kinyago kimoja chenye sura ya tembo na bangili tisa zilizotengenezwa kwa kutumia meno ya Tembo na maganda matatu ya mayai ya Mbuni.

Kamanda Rwambow amesema hadi sasa, thamani halisi ya nyara hizo bado haijafahamika na kwamba upelelezi kuhusiana na mfanyabiashara huyo bado uanendelea.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.