|
Maiti ya mtoto yaopolewa chooni
2007-04-23 19:06:21
Na Kiyao Hoza, Jijini
Maiti ya mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa wa siku tatu imeopolewa chooni Mbagala Kimbangulile, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Kamanda wa mkoa wa kipolisi wa Temeke, Emmanuel Kandihabi, amesema maiti ya motto huyo iliopolewa katika choo cha John, jana mishale ya saa 6.30 mchana.
Akasema mkazi wa Kibaha kwa Mathias, Asifiki Salum, 21, amekamatwa na polisi kuhusina na tukio hilo.
Akasema Asifiki alifanya kitendo hicho wakati alipokwenda kumsalimia dada yake aishie huko Mbagala Kimbangulile, karibu na Shule ya St. Mary.
Kamanda Kandihabi amesema upelelezi ukishakamilika, mtuhumiwa atafikishwa kortini.
|