23 Apr 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wafagiaji wazoa minoti kwenye taka
 
2007-04-23 19:08:12
Na Frankfort

Ama kweli unaweza kulala maskini na kuamka tajiri kama ilivyotokea kwa wana ndoa hawa wanaofanya kazi za ufagiaji na uzoaji takataka kando kando ya barabara.

Siku yao ilianza kama kawaida…baada ya kutua kibaruani alfajiri, walianza kuchapa mzigo kwa kupakua takataka kutoka kwenye mapipa na kuziweka kwenye gari maalum.

Kibarua hicho kikaendelea kwa zaidi ya saa tano. Lakini ghafla, kama zali, mmoja wao akaona kitu, kitu ambacho huenda kikabadilisha maisha yao kabisa.

Tukio hilo la kusisimua limetokea katika mji wa Frankfort, nchini Marekani.

Walioangukiwa na zali hilo wametajwa kuwa ni Bw. Ronnie na mkewe Tina Abbot ambao wakati wanakwaa ngekewa hiyo walikuwa wanafanya usafi kwenye mtaa wa Clinton ulioko Kaskazini Magharibi kwa Indianapolis.

Wana ndoa hao waliokota tiketi ya bahati nasibu iliyokuwa imetupwa kwenye pipa la takataka bila kukwanguliwa.

Kwa kujaribu, waliikwangua na kuamua kuiwasilisha kwenye kibanda cha wachezesha bahati nasibu ili kujaribu bahati yao.

Kesho yake, hawakuamini maskini yao pale tiketi yao ilipotajwa kuwa miongoni mwa zile zilizoshinda kitita cha dola za Kimarekani 1,000, ambazo kwa hesabu za haraka haraka, kiasi hicho kwa pesa za hapa Bongo ni sawa na shilingi Mil. 1.4.

``Kazi ya kuzoa takataka inataka moyo…licha ya kuchosha, hailipi…tunaifanya tu kwa vile hatuna namna, `` Tina alikaririwa akisema baada ya tiketi yao kushinda.

Hata hivyo akasema hadi sasa yeye na mumewe bado hawajaamua ni vipi watatumia kitita hicho ingawa wote wangependa kuanzisha biashara na kufanya shughuli inayolipa.

Wana ndoa hao wakati wanabahatika, walishakusanya takataka kwa zaidi ya saa tano kando kando ya barabara.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.