24 Apr 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Serikali yaifunga sekondari iliyofelisha wanafunzi kibao Jijini
 
2007-04-24 17:28:51
Na Usu-Emma Sindila, Jijini

Wakati serikali ikiwa katika kampeni kabambe ya ujenzi wa shule kwa kila kata ili kuinua kiwango cha elimu nchini, shule moja binafsi ya sekondari Jijini imefungwa kutokana na matatizo kibao yaliyokuwa yakiielemea.

Shule hiyo iliyopo katika maeneo ya Kinondoni, inafahamika kwa jina la Fares Kisingo na imeamuriwa kufungwa kutokana na sababu mbalimbali, baadhi zikiwa ni utovu wa nidhamu wa wanafunzi na pia mmiliki wake kupandisha ada iliyowashinda wazazi wengi wa wanafunzi wa shule hiyo.

Imeelezwa kuwa licha ya mmiliki huyo kupandisha ada, shule hiyo pia imekuwa na idadi ndogo ya wanafunzi na hivyo kupunguza mapato na hatimaye kuendeshwa kwa hasara.

Kama haitoshi, shule hiyo pia imeamuriwa kufungwa kutokana na matokeo yake mabaya ya kidato cha nne mwaka uliopita.

Taarifa iliyothibitishwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kisha kutiwa saini na A.S.M Mwaimu, kwa niaba ya Katibu Mkuu, ilisema kuwa shule hiyo imefungwa toka Februari 28, mwaka huu.

Pia, Wizara imesema imeipiga marufuku shule hiyo kuandikisha wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza mwaka ujao wa masomo huku wale waliopo kidato cha kwanza mwaka huu wakitafutiwa shule nyingine.

Wizara hiyo imesema kuwa inayo taarifa kuwa mmiliki wa shule hiyo anahaha kuwatafutia shule nyingine wanafunzi wa kidato cha pili hadi cha nne, kwa madai kuwa kuwasubiri hadi watakapomaliza mwaka 2009 itakuwa mzigo kwake.

Shule hiyo iliyosajiliwa kwa namba S.1345, ilikuwa na wanafunzi wavulana na wasichana.

Katika matokeo ya mwaka jana ya kidato cha nne, shule hiyo inadaiwa haikuweza kuto amwanafunzi hata mmoja kwenda kidato cha tano ambapo kati ya wanafunzi 66 waliofanya mtihani, 43 walipata daraja la nne na 23 walipata daraja sifuri!

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.