24 Apr 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mwanafunzi `praimari` adakwa kwa ujambazi
 
2007-04-24 17:31:19
Na Janneth Kiure, Kibaha

Jeshi la Polisi mkoani Pwani, linawashikilia watu watatu akiwemo mwanafunzi wa shule ya msingi, kwa tuhuma za ujambazi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Shaibu Ibrahim, amemtaja mwanafunzi huyo kwa jina moja la Kumbusa,19, anayesoma Shule ya Msingi Nyamwage, Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani.

Akasema watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa tuhuma za kuvunja nyumba na kuiba vitu mbali mbali.

Kamanda huyo amesema watuhumiwa hao walikamatwa Aprili 17 mwaka huu, saa 4:00 usiku wakati polisi walipokuwa katika doria.

Akasema watuhumiwa hao wanadaiwa kuvunja nyumba ya Sikudhani Hashimu ,30, mkulima na mkazi wa eneo la Nyamwage.

Akasema watuhumiwa hao wakiwa na silaha za jadi walidakwa na polisi baada ya ushirikiano wa wananchi.

Akasema walikutwa wamejificha porini.
Akawataja wengine kuwa ni Mbwana Omary, Kitambulo, 30, Kiasimu Seif, 35.

Amevitaja vitu vilivyoibiwa baada ya watuhumiwa hao kuvunja mlango kwa kutumia mashoka, mapanga na marungu kuwa ni pesa taslimu Sh. 180,000 na vitu mbalimbali ikiwemo redio moja aina ya Sony yenye thamani ya Sh. 30,000 pamoja na nguo mbalimbali zenye thamani ya Sh. 6,000.

Kwa mujibu wa Kamanda Shaibu, upelelezi uliofanywa na polisi umebaini kuwa baada ya majambazi hayo kuiba walifanikiwa kuziuza mali hizo kwa watu mbalimbali ambao nao wamedakwa.

Akawataja wanunuzi wa mali hizo za wizi kuwa ni Kialimu Seif na mtu mwingine ambaye hakumtaja jina, ambaye alidakwa na redio ya mlalamikaji.

Akasema watuhumiwa hao ni wazoefu katika matukio ya uvunjaji wa nyumba na kuiba mali mbalimbali.

Kamanda huyo akasema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Katika tukio lingine, watu watatu wamesalimisha bunduki wilayani Kisarawe mkoa humo, nje ya nyumba ya Mtendaji wa Kata kijiji cha Vikumburu.

Akamtaja mtuhumiwa huyo aliyebwaga silaha kuwa ni Almasi.
Kamanda huyo akasema mtuhumiwa huyo alisalimisha bunduki aina ya Rifle, yenye namba 72526_03956 ambayo ina Cable namba 3.75.

Akasema upelelezi umebaini kuwa silaha hiyo aliachiwa na marehemu baba yake.
Polisi inamsaka mtuhumiwa huyo ili iweze kumfikisha mahakamani.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.