|
Maendeleo ya Sada
2007-04-24 17:34:49
Na Mwandishi Wetu
Bi. Mwanaidi Mwesi, 17, ambaye aliomba msaada wa pesa kwa ajili ya matibabu ya mtoto wake, Sada anatarajia kupokea pesa zilizochangwa hadi sasa leo katika ofisi za gazeti hili zilizoko Mikocheni, Jijini.
Mama huyo alitua Jijini jana jioni akitokea Moshi baada ya kupewa taarifa kwamba wasamaria wema wamemchangia fedha kwa ajili ya matibabu ya mwanae.
Mtoto Sada anasumbuliwa na matatizo ya kupumua baada ya kuzaliwa bila kuwa na pua, hali hiyo imemfanya aishi kwa shida kubwa huku mama yake akiwa hana msaada wowote.
Baba yake Sada alitimka baada ya mkewe kujifungua mtoto mwenye matatizo ya kiafya.
|