24 Apr 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mama aua mwanawe
 
2007-04-24 17:36:35
Na Janeth Kiure, Pwani

Mama mmoja wilayani Kisarawe anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumcharaza bakora mwanawe wa kumzaa hadi kumsababishia umauti.

Mama huyo, ametajwa kwa jina la Aisha Mussa, mkazi wa Zegero, tarafa ya Mzenga mkoani Pwani, anadaiwa kumuua mwanawe Habib Kayaya kwa `mboko` za mti uitwao `mdudume`.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Shaibu Ibrahim, amesema tukio hilo limetokea Aprili 20 mwaka huu, mishale ya saa 7.18 mchana.

Akasema mtuhumiwa huyo alimchapa marehemu mwilini katika sehemu za bega, shingo, kichwani na kisogoni.

Akasema kabla ya kukutwa na umauti huo, marehemu alikwenda nyumbani kwa mzazi wake huyo akiwa amelewa chakari na kuwataka wampatie fedha alizowapa kwa ajili ya kununulia chakula.

``Kama ilivyo kawaida yake anapolewa, marehemu baada tu ya kufika nyumbani, alianza kuwatukana na kuwapiga wazazi wake,`` akasema Kamanda Ibrahim.

Akasema kutokana na tabia hiyo, mama yake aliamua kuchukua fimbo na kumcharaza nayo ili kujisalimisha na bughudha hizo na ndipo umauti ukamkuta kijana huyo.

Akasema mwili wa kijana huyo umeshafanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi.

Akasema mama anayetuhumiwa kwa mauaji hayo, ameshakamatwa na atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.