30 Apr 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Guluka Kwalala kukabidhiwa zahanati yao mwezi Julai
 
2007-04-30 15:49:24
Na Claudia Kayombo TSJ

Jengo la zahanati ya Guluka Kwalala linalofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii,TASAF, linatarajia kukamilika mwezi Julai mwaka huu.

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa huo, Bw. Charles Mnuona, amesema jengo hilo lipo katika hatua za kuezekwa, wakati vyoo navyo vipo katika hatua za mwisho za ujenzi.

Akizungumzia kuhusu mchango wa asilimia 20 wanazotakiwa kuchangia wakazi wa mtaa huo, ambao awali ulikuwa unasuasua, amesema hivi sasa kuna mabadiliko makubwa kwani wakazi hao wamekuwa wakijitokeza kwa wingi katika kuchangia ujenzi huo.

Akasema hali ngumu ya kiuchumi iliyopo kwa sasa ni miongoni mwa sababu chache zilizosababisha kusuasua kwa michango hiyo.

Hata hivyo akasema, kutokana na kusuasua kwa michango hiyo uongozi wa mtaa huo pamoja na kamati ya ujenzi, waliafikiana kubuni njia nyingine ya kufanikisha michango huo.

Akasema kamati hiyo ilibuni kuwa kila mwananchi anayefika kupata huduma katika ofisi ya mtaa huo, kuchangia Sh. 3,000.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi huo, Diwani mstaafu, Bw. Samwel Marwa, amesema hadi sasa wananchi wamechanga zaidi ya Sh. 300,000.

Gharama za ujenzi huo zinatarajia kuwa zaidi ya Sh. Milioni 56 hadi kukamilika ambapo wakazi wa mtaa huo wanatakiwa kuchangia Sh. Milioni 9.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.