12 Jun 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Zanzibar yavuka lengo la ukusanyaji kodi kwa mwezi
 
2007-06-12 16:33:46
Na Moris Lyimo, Jijini

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekusanya jumla ya shilingi bilioni 8.2 na kuruka lengo la kukusanya bilioni 7. 2 kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato katika kipindi cha mwezi Machi Mwaka huu.

Taarifa ya hali ya uchumi ya kila mwezi inayotolewa na Benki Kuu ya Tanzania, imesema ongezeko hilo ambalo ni sawa na asilimia 13.9, imetokana zaidi na ongezeko la bidhaa zinazoingizwa nchini na kodi za bidhaa.

Pia ongozeko hilo ni kutokana na ongezeko la marejesho ya mapato ya kodi, uhusiano kati ya wakala wa ukusanyaji kodi ambao ni Mamlaka ya Mapato nchini, TRA na Bodi ya Mapato Zanzibar, ZRB.

Inasema taarifa hiyo kuwa viwango vya kodi katika kipindi hicho ilikuwa ni Shilingi Bilioni 1.6 iliyotokana na makusanyo ya kodi za bidhaa zinazoingia na kuzidi lengo la bilioni 1.4 zilizotakiwa kukusanywa kwa kipindi hicho.

Kodi ya ushuru wa forodha imechangia Sh. Bilioni 2.4 na kupita lengo la Sh. Bilioni 2.2, hivyo kufanya makusanyo ya kodi katika eneo hilo kufikia asilimia 33.3.

Pia hali nzuri ya makusanyo y visiwani humo katika kipindi hicho yametajwa kuwa ni kutokana na hali nzuri ya kodi ya sekta ya utalii na marejesho kutoka bara.

Taarifa inaendelea kueleza kuwa kodi ya mapato iliyokusanywa ni kiasi cha Shilinghi Bilioni Moja juu ya lengo la kukusanya mapato ya aina hiyo ambayo yalikuwa ni Sh. Milioni 900 yatokanayo na marejesho ya kodi ya mapato wakati makusanyo mengine yalifikia Sh.Bilioni 2.1 na kuzidi lengo la kukusanya Sh. Bilioni Mbili.

Mapato yaliyotokana na taasisi zisizolipa kodi yalikuwa Sh. Milioni 900 ambayo ni juu ya lengo la Sh. Milioni 500 zilizotokana na ongezeko la makusanyo ya wizara na kufikia asilimia11.0 ya mapato yote.

Benki Kuu imeongeza katika taarifa yake hiyo kuwa kwa kipindi cha Julai mwaka jana hadi Machi mwaka huu, makusanyo yalifikia Sh. Bilioni 67.6, hivyo kupita lengo la makusanyo ya sh. Sh. Bilioni 65.5 kwa asilimia 2.1.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.