12 Jun 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Daladala yavaa gari la polisi
 
2007-06-12 16:36:59
Na USU-EMMA SINDILA FUTUNA SELEMANI, JIJINI

Watu 23 wa Jijini Dar es Salaam wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwemo maarufu kama daladala kuvaana na difenda la polisi.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Emmanuel Kandihabi amesema ajali hiyo ilitokea jana saa 7:25 mchana kwenye makutano ya taa za kuongozea magari za Chang\'ombe na Mandela.

Amesema daladala hiyo iliyokuwa imejaa abiria ni Isuzu inayopiga ruti kati ya Tandika na Kariakoo, iliyokuwa ikiendeshwa na Ernest Philemon.

Amesema gari la polisi lililohusika katika ajali hiyo ni PT 0008 Leyland lililokuwa likiendeshwa na askari mwenye namba D 3491 anayejulikana kama Sajenti Thomas.

Kamanda Kandihabi amesewataja baadhi wa watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Salum Mkenengene, Rose Mzinduka, Hamis Ramadhani, Esta Mushi na Juma Ally.

Amesema majeruhi wote 23 wametibiwa katika hospitali ya wilaya ya Temeke na kuruhusiwa.

Katika tukio jingine kamanda Kandihabi amsema mtu mmoja amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kamba ya manila aliyoifunga katika nguzo za ghorofa ya pili kwenye kota za polisi Kurasini.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Emmanuel Kandihabi, amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo saa 8:15 huko kota Mivinjeni, Kurasini.

Amemtaja mtu huyo kuwa ni Abdalah Mashauri, 40, ambaye ni kaka wa askari wa Jeshi la Polisi, katika kituo cha Wazo Hill, aliyetambulika kwa jina moja la Salum.

Amesema chanzo cha mtu huyo kujinyonga hakijafahamika na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo unaendelea.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Temeke.

  • SOURCE: Alasiri
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.